23/07/2011

Mhariri Mwakiteleko afariki Dunia

Danny Mwakiteleko
Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Danny Mwakiteleko, amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kabla ya kufariki, Mwakiteleko alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi Hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia ajali ya gari aliyoipata Jumatano usiku, eneo la Tabata (ToT). 

Inaelezwa kuwa ajali iliyogharimu maisha ya Mwakiteleko ilitokea baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongwa na lori lenye trela majira ya saa nne usiku na baadaye lori hilo kutoweka. Mwakiteleko alipata ajali hiyo akiwa anatokea ofisini Sinza Kijiweni yaliko makao makuu ya kampuni ya New Habari (2006), ambapo inaelezwa alifanya kazi  hadi saa tatu za usiku. 

Kabla ya kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwakiteleko aliwahishwa Hospitali ya Amana ambapo madaktari waliamua apelekwe Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi. Taarifa kutoka kwa madaktari wa kitengo cha upasuaji (MOI) zilieleza kuwa Mwakiteleko aliumia kichwani na kumfanya apoteze fahamu kiasi, hali iliyolazimisha kufanyiwa upasuaji sehemu ya kichwa kwenye paji la uso. Rais Jakaya Kikwete alikwenda Hospitali ya Muhimbili jana kumjulia hali na kuelezwa kuwa hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.  

Mhariri Mwakiteleko atakumbukwa kwa upole wake, uchapakazi na juhudi zake katika kuendeleza tasnia hii ya habari. Mungu amlaze mahali pema peponi Mhariri Mwakiteleko. Kibaraza hiki kinatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Mhariri Mwakiteleko.

2 comments:

  1. Poleni sana, tena saaana saaana!

    Kupoteza mchapakazi ni pigo kubwa katika jamii yoyote. Lakini kupoteza mwandishi mchapakazi ni jelaha kubwa katika taifa lolote lile.

    Labda hawa watu wanahitaji wakuendesha magari yao SHOFEYI kwa sababu huwezi ukafanya kazi ya akili hadi usiku kisha uwe na uwezo kamili wakuendesha gari... mishipa ya fahamu imechoka.


    Nasikia hata mwalimu wangu shuleni ya Uandishi Wa Habari Tanzania, Marehemu Bw Bwire Masatu Musalika, aliiifariki dunia hivyohivyo miaka mingi iliepita lakini.Kamanda mkuu wa jeshi la chama cha ukombozi Afrika Kusini, Sabelo Phama naye aliendesha gari mwenyewe kutoka Dar kwenda Moro wakati gari lake lilipoingia chini yaTRUCK na kumtoa roho papo hapo.

    Vifo vya watu barabarani havisameheki kwangu kwa kuwa HAVIKUANDIKWA! (Ni bora zaidi roho ya mtu kutolewa na mtu mwingine kuliko gari). Kwa hiyo lazima jamii yetu ibadili namna tunavyotumia magari.

    Asante kwa kututaarifu, Mkuu!

    ReplyDelete
  2. Shukrani, umenena yote kamanda GMP!

    ReplyDelete