Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akitoa tamko la msimamo wa serikali kuhusu shughuli zilizokuwa zinaendeshwa na Kampuni ya Deci (Tanzania) Limited.
SIKU chache baada ya kusimamishwa shughuli za Taasisi ya Development Enterpreneurship Community Initiative (Deci), serikali imetangaza kufunga akaunti zote za wamiliki wake na kudhibiti maeneo yote ya shughuli za taasisi hiyo kwa lengo la kuwezesha kurudisha fedha kwa wananchi.
Tamko hilo la Serikali limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo katika mkutano na waaandishi wa habari makao makuu ya wizara hiyo huku waziri huyo akiwaweka waandishi ukumbi wa mikutano kwa zaidi ya saa moja na nusu kumsubiri.
Kauli hiyo ya Serikali imekuja wakati wanachama wa taasisi hiyo wakiwa katika hali tata kutojua hatima ya mbegu zao walizopanda wakati wakisubiri hatima ya uchunguzi wa serikali.
Waziri Mkulo aliyeelezwa kuanza mkutano saa sita na robo, mchana aliingia ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo saa 7. 48 na kueleza kuwa " Tamko nitakalolitoa ni zito na muhimu, limepitiwa na kukubaliwa na Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais. Mimi natoa tamko la serikali kama waziri kwa ababu shughuli za taasisi hiyo zinaihusu wizara yangu ya Fedha na uchumi:
"Ilibidi wakubwa walipitie na kuidhinisha, ni tamko linalojitosheleza kwa kila hali, lina kurasa 21, lakini hapa nimefupisha hadi kufikia kurasa tatu,"alisema Mkulo.
Alisema Deci imeamua kusitisha shughuli zake hatua ambayo imesababisha wasiwasi mwingi miongoni mwa wanachama wake na kwamba serikali imeamua "Kuhakikisha maeneo yote ya shughuli za Deci yanadhibitiwa, kukinga pesa zote zilizopo katika akaunti za waendeshaji wa Deci na Deci yenyewe hadi hatma ya shughuli za Deci itakapojulikana."
Waziri Mkulo alibainisha kuwa "Serikali inaendelea na hatua za kuhakikisha waendeshaji na wamiliki wote wa Deci hawatoroki."
Kwa undani zaidi bofya hapa
Wadau Mnasemaje juu ya hatua hii ya serikali?
Hodi kibarazani nimepita kusalimia nimekuona kwa dada Koero.
ReplyDeleteKaribu Dada Yasinta,
ReplyDeleteKaribu bila kusita
Furaha mgeni kupata
Kwangu baraka kuweka
Kwako huwa naingia
Maisha barazania
Link nimekuwekea
Waweza ona kulia
Tuendeleze libeneke
Ukweli uelezeke
Nia zetu tuziweke
Nchi tuiezeke!
Nami nimekuona kwa Da Koero nikaona nijiunge kukukaribisha. Asante kwa kuwa nasi na kutuweka kwenye list ya magazeti tando. Nami nitafanya hivyo kwangu na nitashiriki mijadala endelevu iliyopo hapa kwa kadri ya uwezo wangu.
ReplyDeleteKaribu na KARIBU SANA
Ahsante sana mzee wa changamoto!
ReplyDeleteTupo pamoja na jiko na moto!
Sijui nimepotea njia......
ReplyDeleteHivi niko wapi hapa............Duh!!!!1
Aaaahh!!!!! Sijapotea.......
haya mwenye mji huu upoooo!!!!!!
Nimepita hapa namtafuta kuku wangu sijui nimemkuta?
habari za siku kaka, mzee wa sosholojia,
nilikuwa na pilika pilika za hapa na pale lakini leo alfajiri nimepita hapa kukusalimia nikielekea shamba.
haya nikirudi nitapita kukujulia hali......
Karibu tena VUKANI.....
Dada Koero hujapotea,hapa ni kwangu nyumbani
ReplyDeleteJiwe niliegemezea, nikaingia chumbani
Sautiyo ikipenyea, hodi hodi humu ndani
Karibu dada Koero, kuku wako nilimuona
Kuku wako nilimuona, akila mchangani
Kwa kuwa anajulikana, hapa kwangu nyumbani
Rangi zake nzuri sana,anashika usukani
Karibu dada Koero, kuku wako nilimuona
Nashukuru umeahidi, kunipitia ukirudi
Unibebee na mahindi, VUKANI unaporudi
Nami nakuahidi, kwako nitabisha hodi
Karibu dada Koero, kuku wako nilimuona
Haya nimerudi Shamba na kwa bahati mbaya sijakukuta, ila nimemkuta mwanao, kijimzigo chako cha mahindi nimeegemeza hapo upenuni, kuku wangu nitamfuata kesho nimeambiwa na mwanao kuwa anatamia.
ReplyDeleteMwaka huu naona mvua za vuli zimechelewa....sijuia ndio ule mwaka wa njaa ushaanza?......haya ukila ukumbuke kuweka akiba
Dada Koero ahsante sana, kijimzigo nimekipata
ReplyDeleteKidogo tu tumepishana, mwanangu kanifuata
Nilikwenda kumuona, Mzee Masulupweta
Nimekuta analia sana, huku moyo wampwita
Anasema hana amani, kapoteza fedha zake
Amepanda mbegu shambani, kabana mifuko yake
Amekuta miba shambani, katika mipaka yake
Masulupweta analia sana, huku moyo wampwita
Mimi nikamfariji, ajikaze kisabuni
Hata nikampa uji, pale kwake upenuni
Asikimbilie jiji,kule serikalini
Masulupweta analia sana, huku moyo wampwita
Wakati nikimliwaza, mwanangu alinijia
Ndipo akaninong'oneza, mgeni katupitia
Upepo nikaukimbiza, nyumbani kufikia
Dada Koero nashukuru sana, kijimzigo nimekipata
Mfikishie pole zake huyo Mzee Masulupwete,
ReplyDeleteMwambie asikate tamaa, kwani kila baya nyuma yake kuna zuri limefichama....