Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha daladala wakaanza kufanya mazungumzo. Mmoja aling'ang'nia kuzungumzia kero zinazoikabili familia yake, mwenzie akimsikiliza kwa makini, na hatimaye mwenzake (jamaa wa pili) naye akasema 'Wewe unadhani familia yako ina matatizo makubwa swahiba? ...Hayo yote ni cha mtoto kwa haya ya kwangu nitakayo kupasha hivi punde!!'
Basi hebu nisikilize:
'Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekuwa na binti mmoja mkubwa tu aliyemzaa na tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akaja kumuoa huyo binti yangu wa kambo , hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume, ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.
Baadaye baada ya mwaka hivi kupita huyu binti ya mke wangu, yaani binti yangu wa kambo alifanikiwa kupata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume alikuwa ndugu yangu kwa sababu tulichangia baba mmoja, lakini kwa vile alikuwa ni mtoto wa binti wa mke wangu, papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake ndogo wangu. ..Upo hapo swahibaa!!.
Lakini hayo yote yalikuwa si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipokuja kupata mtoto wa kiume. Sasa mke wa baba ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyu wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kuwa shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndiye mke wa baba yangu.
Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa binti yake mwenyewe!! Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe'.
SWALI;
'Je, unadhani mpaka hapo wewe una matatizo ya kifamilia? Acha kulalamika kwa vijisenti vya matatizo wenzio wana mabilioni ya matatizo bwana!!!!!
No comments:
Post a Comment