22/06/2009

Pigo la Mwaka: Mama Yangu Ameaga Dunia

Jeneza lililohifadhi mwili wa mama

Familia ikiomboleza, mjukuu wa marehemu mama, binti yangu Magreth akiwa amefumbata mikono katika lindi la mawazo

Nilishindwa kujizuia kutoa machozi kwa uchungu baada ya kuiona sura ya mama kwa mara ya mwisho

Baba yangu akiaga mwili wa mkewe

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu mama likishushwa kaburini

Niliweka shada la maua katika kaburi la mama

Kimya hiki kingine kimesababishwa na msiba mkubwa niliopata. Tarehe 16 mwezi huu, siku ya Jumanne, mama yangu mzazi aliaga dunia katika hospitali ya Mission Mikocheni, Dar es Salaam. Pamoja na jitihada zote za kuokoa maisha yake, mama alifariki saa mbili asubuhi.

Tulimzika mpendwa wetu tarehe 18, katika makaburi ya City, Yombo Dovya na kuendelea na kipindi cha maombolezo. Lazima niwe mkweli, nimempoteza mtu muhimu sana maishani mwangu, nafahamu fika kuwa ni lazima sote twende mbele ya haki, kwa vipindi na nyakati tofauti, lakini sikutegemea kama hili lingetokea kwa sasa. Faraja pekee niliyonayo baada ya msiba huu ni kwamba, nimeweza kuonana na mama baada ya kurudi toka Dublin (wengine wanasema ni kama alikuwa ananisubiri!).

Nitajitahidi kuyaenzi mazuri aliyoniachia na kunifanyia mama, kama ishara ya kuthamini mchango wake kwangu. Mama alipenda sana nipate elimu, na alinisaidia kivitendo. Naliona jukumu kubwa mbele yangu la kuwasaidia wengine kama ambavyo mama alifanya kwangu.

19 comments:

  1. Kaka yetu pamoja na familia yako poleni sana kwa msiba huu mzito,tupo pamoja katika sala na Mwenyezi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi kigumu cha majonzi. Apumzike kwa amani

    ReplyDelete
  2. Mwanasosholojia pole tena pole sana nakuelewa kabisa uchungu ulionao leo Kwani kuondokewa na MAMA.Marehemu astarehe kwa amani. Amina

    ReplyDelete
  3. Pole sana kwa kufiwa na Mama yako mzazi.Mwenyezi Mungu akupe nguvu katika wakati huu mgumu kwako.
    Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mama mahali pema peponi.Amen.
    Mdau
    Faustine

    ReplyDelete
  4. Poleni sana na msiba jamani,namuomba mwenyenzi awape nguvu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi.Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya marehemu Mama mahali pema peponi.Amen.

    ReplyDelete
  5. Pole sana ,Mwanasosholojia.Pumziko la milele ampe Bwana na Mwanga wa Milele Amuangazie,Apumzike kwa Amani,Amen.

    ReplyDelete
  6. Narudi tena nimeona picha pole sana kakangu. Tumwombee mama hicho ndio kikubwa. Nipo nawe katika maombolezo.

    ReplyDelete
  7. Ni mangapi twaweza kusema kufariji kuondokewa na Mama? HAKUNA. Lakini kuna tunayoweza kuyafanya kumuenzi Mama ambaye alikupenda sana Mwanasosholojia.
    Mama alitenda iliyo sehemu yake na sasa amepumzika. Nasi tutaendelea kuenzi mema aliyokuelekeza kwa kusoma na kuyatekeleza toka kwako.
    Mama yu-nasi kiroho na twapaswa kuenzi mema yake.

    ReplyDelete
  8. Pole sana Kaka. Na poleni sana wanafamilia. Tuendelee kumwomba Mungu ampumzishe mama yetu mahali pema AMINA. "Bwana alitoa na Bwana ametwaa.Jina la Bwana libarikiwe" Ayubu 1:21

    ReplyDelete
  9. Pole sana Ndugu yangu, Mungu akupe Nguvu pamoja na Familia yako kukabiliana na pigo lililokupata. Mungu Ailaze roho ya Marehemu mahali pema Peponi. Amin.
    Tram

    ReplyDelete
  10. Pole sana kaka kwa msiba huu mkubwa,hakika hakuna kama mama,mshukuru mungu kwa kukuwezesha kwenda kumuona mama bado akiwa hai,hiyo ni faraja kubwa kwako,tumuombee kwa mungu amuweke mahali pema.

    ReplyDelete
  11. Kweli hili ni pigo la mwaka. Pole sana na Mungu akupe nguvu wewe na familia yako katika kipindi hiki cha uchungu. Mungu ampe mama pumziko jema!

    ReplyDelete
  12. Poleni sana kwa msiba huu mzito ukichukulia kuwa mama ndio nguzo ya familia, bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

    ReplyDelete
  13. sijui niseme nnini maanake kwa kiasi kikuuubwa natofautiana na woooote walionitangulia. nivyma nikae kimya nisije onekana namnagani vipi hapa labda nnijiunge kusema polesana utadhani namaanisha vile na labda tujiaminshe tu kuwa mama yako kakuachia pengo lsilozibika!!!

    polee

    ReplyDelete
  14. Najisikia simanzi kubwa kuchelewa kuisoma tanzia hii. Walotangulia wamesema. Nami naungana na wadau wengine kukupa pole nyingi. Namwomba Mwenyezi Mungu akupe faraja.
    Pia aipokee roho ya mama na kuiweka mahala pema.
    Pole sana mkuu.

    ReplyDelete
  15. Pole sana kwa msiba uliokupata

    ReplyDelete
  16. Pole sana Mathew. Ni msiba mkubwa sana. hiki ni kipindi kigumu kwako, lakini ni wajibu wetu kupokea mapenzi ya Mungu. "Be Strong and of Good courage"

    ReplyDelete
  17. Pole sana Mwanasosholojia. Nimechelewa sana kuisoma tanzia hii.

    ReplyDelete
  18. Nawashukuru sana ndugu zangu nyote!

    ReplyDelete