
Ninakupenda mpenzi, ulonijaa moyoni
Daima nitakuenzi, siku zote maishani
Nakutungia utenzi, uelewe ya rohoni
Nipo kwa ajili yako, ewe wangu maabuba
Hainipiti dakika, bila kukufikiria
Sikufanyii dhihaka, ukweli nakuambia
Umeniteka hakika, mpenzi nakuapia
Nipo kwa ajili yako, ewe wangu maabuba
Nikosapo kukuona, moyoni ninaumia
Mpweke ninajiona, uchungu nagugumia
Mara tu nikikuona, furaha inanijia
Nipo kwa ajili yako, ewe wangu maabuba
Tunapokuwa pamoja, wanipa raha hakika
Tumeujenga umoja, ewe wangu malaika
Tusivifanye vioja, penzi letu kuvunjika
Nipo kwa ajili yako, ewe wangu maabuba
Daima nakutunzia, hili penzilo mwanana
Moyoni nakuwekea, usipate shaka sana
Popote napoelekea, usiku hata mchana
Nipo kwa ajili yako, ewe wangu maabuba
Shairi limetulia kweli kaka nadhani uliyemtungia atafurahi au amefurahi kweli.
ReplyDeleteWewe ni langu chaguo, mwinginewe sijamwona,
ReplyDeleteWewe si sawa na nguo, na mwingine kufanana,
Upendo wangu ni huo, kwingine kote hakuna,
Hakika nitakuenzi, kwa maisha yangu yote!