17/04/2013

Kurejea Rasmi!


Ni takribani miezi mitano sasa imepita tokea kubandikwa kwa "bandiko" la mwisho katika kibaraza chetu hiki. Tena "bandiko" lenyewe liliwekwa baada ya "ka-muda" fulani kupita! Hii yote ilitokana na sababu ambazo hazikuweza kuepukika, zilizopelekea kukosekana kabisa hata "ka-upenyo" kubandika chochote.

Kipindi chote hiki hakika kilikuwa kinarindima sambamba na hamu ya kurejea rasmi kibarazani. Hamu hii ikitangulizwa na nia na mikakati ya kuboresha zaidi kibaraza chetu, kuhakikisha kuwa pamoja na mambo mengine, kutokosekana kabisa kwa "mabandiko".

Kwa maneno hayo machache kwa sasa, Mwenyekiti anatangaza kurejea rasmi kwa kibaraza chetu.

1 comment:

  1. Duh! Mwenyekiti karibu sana sana maana ulimisiwa kwelikweli. Natumaini ulichokuwa ukifanya umefanikiwa:-)

    ReplyDelete