22/05/2009

Eti Omba Omba Wapo Afrika tu!

Kuna watu huwa nawasikia wanasema kuwa sisi wabongo tumezidi kuwa omba omba. Na wengine hudiriki hata kusema kuwa tunatia aibu kwa wageni kwa kuwa na omba omba a.k.a Matonyazz kibao mitaani bongo. Mimi (na pengine hata wadau wengine) nshawaona omba omba a.k.a Tonyazz wa kidhungu mamtoni. Wapo tena wamejaa tele kama pishi la mchele katika mitaa mbali mbali, na wanatumia staili ile ile ya omba omba wetu wa bongo. Kuna wale wanaotumia staili ya mzee wetu omba omba maarufu toka Idodomya (Matonya) ambae aliasisi jina hili kwa omba omba wote. Kuna wengine ambao wanatumia staili ile ya wale wa makutano ya barabara na kwenye mataa ya kuongozea vyombo vya usafiri (Trafikilaitsi). 

Wadau hebu wacheki hawa Tonyazz wa kidhungu niliobahatika kuwakon'goli picha;

Tonya wa kidhungu akiwa ameshika kijikopo chake akiomba chochote mtaani Dublin, Ireland

Tonya mwingine akiiga ile staili ya mzee Matonya wa Bongo, kibaridi kinamchapa kajifunika miguu na kipande cha nguo, hapa ni kama anamcheki kwa uchungu huyu mdada aliyepita bila kumpa chochote!

Wadau si mmecheki matonyazzz si Bongo tu, hapa kwa hawa jamaa wapo!!

4 comments:

  1. nIMEFURAHI SANA KWA KUIWEKA MADA HII HAPA KIBARAZANI nilikuwa natarajia kuandika hilo kwa kweli huwa naumia sana watu wanavyoishusha Afrika yetu. Hata sijaelewa ni kwanini? Yaani acha tu kuna waomba omba huku kiasi kwamba unaweza kuogopa kwenda nje. Na wengine wanaomba kwa njia ya kupiga miziki barabarani. Huwa nimesema mara nyingi katika blog yangu Afadhali kuishi Afrika utakwenda kwa jirani na ukaomba chumvi au unga na ukala. Lakini huku kila mtu kalumanyile nadhani ndi maana kuna waombaji wengi zaidi.Ni hayo tu isije nikaandika yote na wengine wakakosa kusema. Asante

    ReplyDelete
  2. Shukrani kwa maoni da Yasinta!

    ReplyDelete
  3. tembea uoneee, naam, ombaomba wapo pote duniani

    ReplyDelete
  4. Naaam, tembea uone. Omba omba wapo kila mahali, hata wadhungu waokota vyakula majalalani wapo

    ReplyDelete