20/05/2009

Usafi wa Barabara na Teknolojia!


Wakati Bongo manispaa zetu bado zinatumia nguvu kazi watu katika kufanya usafi wa barabara (huku wengi ambao huwa nawaona barabarani wakiwa akina mama wazee), wenzetu mamtoni wanaendelea kuitumia teknolojia ya magari ya kusafisha barabara (kwa kidhungu Road Sweepers). Inavutia, lakini mwezenu najiuliza swali moja...Ni kwa kiasi gani bongo tunaweza kuitumia teknolojia hii kwa sasa? Barabara zetu hizi za vumbi na makorongo kama mashimo ya kuchimbia  madini! Hata kwa zile barabara kuu za lami, manispaa zetu zinaweza kweli kununua magari haya na yakafanya kazi kwa ufanisi kama ilivyo kwa wenzetu? Au hii itawanyima ajira hawa wavuja jasho wanaofanya usafi kwa "fagio chelewa" na kulipwa ujira mdogo pasipo kuzingatia afya zao? Maswali lukuki....! 

Hebu mdau dekshia wenzetu mamtoni walipofikia; 

Hapa jigari la kufanyia usafi likikatiza katika mtaa kufyonza mavumbi na uchafu mwingine 

Lijigari kwa ukaribu zaidi

Lifagio (sio la chelewa) likikusanya uchafu na kisha kufyonzwa na lijigari hili, dereva kazi yake kuendesha na kubofya tu!

Wadau imekaaje hii?

2 comments:

  1. Nimekuwa najiuliza swali hili kwanini isiwe hivi kwetu pia lakini ni kweli pia labda hao wanaofagia watakuwa hawana kazi. Na ndio ni hatari sana kwa afya zao. Halafu kaka umenikumbusha pia kuhusu huu usafi mwaka huu tulipokuwa nyumbani mtoto wangu alikuwa amekula ndizi na baadaye alilishika lile ganda la ndizi na kutafuta sehemu ya kutupa taka lakini hakuona na binamu yake akamwambia atupe tu popote alikataa. Na alilikamata mpaka tuliofika nyumbani. nimekumbuka tu

    ReplyDelete
  2. Kwanza barabara zetu za bongo zilivyo mmmhh,pili hao wanaofagia watakosa kazi.Kikubwa zaidi ni kuzitengeneza barabara si unaona road za wenzetu zilivyobomba.

    ReplyDelete