17/04/2011

Tamaduni Zetu!

Hawa ndugu zetu ni wa kabila la wa-Dani (wengine pia wanaita Ndani) kutoka katika bonde la Baliem, Irian Jaya, Papua-New Guinea. Utamaduni wao umekuwa ukivutia watalii wengi wanaopenda kwenda kuwatembelea na kupiga nao picha (sijui mapato ya utalii huo yanawanufaisha nini wao kama kabila).Wanapofiwa na ndugu wao hukata vidole vyao vya mikono. Inasemekana kabila hili lilitambulika miongoni mwa wageni mnamo mwaka 1938 wakati rubani wa kizungu Richard Archbold alipofika kwa mara ya kwanza katika bonde refu wanamoishi lililozungukwa na milima inayofikia urefu wa mita elfu nne.
Mmoja wa watalii akiwa na wanaume wa kabila la Dani
Ndani ya utamaduni
"...pamoja na ufupi wetu tunazo za saizi zote..."
"...haisumbui, nipo safi kabisa...si mwenyewe unaniona..."
"...tunaanzia mbali...toka tukiwa watoto..."

No comments:

Post a Comment