13/07/2011

Taswira za Prince William na Kate Ziarani

 Baada ya ndoa yao iliyovuta hisia za watu wengi duniani, Duke na Duchess wa Cambridge, Prince William na mkewe Kate bado wamekuwa wakifuatiliwa na wengi. Kimtazamo, huenda wengi wanapenda kuona maisha yao yanakwendaje hasa baada ya ndoa. Vyombo vingi vya habari na mitandao duniani pia vimekuwa vikiwafuatilia. Kate amekuwa chanzo cha habari katika mitandao, majarida na vituo vya Redio na Television katika siku za karibuni kutokana na aina ya mavazi anayovaa.

Hivi punde, Prince William na Kate wamerejea Uingereza kutoka katika ziara yao ya siku kumi waliyoifanya katika nchi ya Canada na mji wa Los Angeles. Kibaraza hiki kinakudondoshea baadhi ya taswira za ziara hiyo kama zilivyotolewa na Associated Press (AP)


 
Prince William na Kate, wakiwa na  Waziri Mkuu wa Canada, Stephen Harper na mkewe Laureen eneo la War Memorial mjini Ottawa, Canada, katika siku yao ya kwanza ya ziara rasmi ya Canada na Marekani, tarehe 30, Juni, 2011 

Wakiwa wameinamisha vichwa kwa muda katika eneo la National War Memorial, Ottawa, Canada.  


Wakicheka baada ya kusaini kitabu cha wageni, Julai 1, 2011, Gatineau, Canada.

Prince William na Kate walipotembelea Maison Dauphine, mjini Quebec City Jumapili ya Julai 3, 2011. Maison Dauphine inatoa hifadhi na huduma kwa familia na watoto walio katika mazingira magumu.

 
Kate (anayeonekana kulia) akishindana katika mbio za boti, Dalvay-by-the-Sea kisiwa cha  Prince Edward, Julai 4, 2011.

 
Prince William, akicheza mpira wa magongo, mjini Yellowknife, Northwest Territories, Canada, Jumanne, Julai 5, 2011.Wa pili kulia anayemuangalia ni mkewe Kate.

 
Prince William na Kate, wakimuangalia binti aliyekuwa akicheza mchezo wa asili, mjini Yellowknife, Northwest Territories, Canada. 

 
Prince William na Kate,  wakizunguka kwa kutumia mtumbwi ziwani Blatchford, Canada.

Duchess wa Cambridge, Kate, akiwapungia mkono watu huko Slave Lake, Alberta, Canada.


Kate akimkumbatia mtoto mwenye miaka sita anayesumbuliwa na kansa, Diamond Marshall baada ya kupewa zawadi ya ua, walipowasili uwanja wa kimataifa wa ndege wa Calgary, Canada.

 
Prince William na Kate, wakiangaliana wakati wa gwaride la heshima waliloandaliwa mjini Calgary, Canada.

 
Prince William and Kate wakipunga mikono kuaga kabla ya kuondoka kwa ndege mjini Calgary, Alberta.

 
Prince William and Kate, walipowasili kwa ajili ya mechi ya hisani ya Polo, Santa Barbara Polo & Racquet Club,Carpinteria, California, Jumamosi ya  Julai 9, 2011. Tukio hilo liliandaliwa kusaidia The American Friends of The Foundation of Prince William and Prince Harry.

 
Prince William na Kate, wakiweka alama za mikono yao katika mchanga huku wakiangaliwa na wanafunzi, wakati wa ziara yao Inner City Arts Academy, Los Angeles, Jumapili ya Julai 10, 2011, Kusini mwa California. 

 
Prince William na Kate, walipowasili Belasco Theatre, Los Angeles wakati wa tukio la uzinduzi wa BAFTA Brits to Watch 2011,  Jumamosi ya Julai 9, 2011.

 
Prince William na Kate,  "wakikwea pipa" ili kuondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles, baada ya kuhitimisha ziara yao ya Marekani. 

No comments:

Post a Comment