18/09/2011

Hongera Daktari Julie Makani!


Daktari Julie Makani

Kufuatia habari za Mwanasayansi na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Cha Tiba na Sayansi za Afya Muhimbili, Daktari Julie Makani kupewa tuzo  na taasisi ya Royal Society Pfizer ili kufanya utafiti wa ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell) Tanzania, kibaraza hiki kinachukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati. Kibaraza kinaamini kuwa juhudi na mchango wa Daktari Makani katika tafiti mbalimbali za magonjwa kama haya zinatambulika namna hii na ni chachu katika kuatafutia ufumbuzi magonjwa yanayoendelea kusumbua jamii yetu.

Habari kwa undani juu ya tuzo hii gonga HAPA


1 comment:

  1. ANGELA JULIUS03/10/2011, 14:14

    HONGERA SANA DADA JULIE MAKANI. NAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA MAISHA YAKO.

    ReplyDelete