22/02/2012

Kumbukumbu

  Mdau wa kibaraza cha Mtoto wa Kitaa, Salum Suleiman Lyeme a.k.a Sule Junior, pamoja na wanafamilia, wanaadhimisha kumbukumbu ya marehemu mama yao. Kibaraza hiki kinaungana na familia katika maadhimisho ya kumbukumbu hiyo.
 

Ni miaka 23 sasa tangu umetutoka lakini sisi kama watoto wako pamoja na baba ulietuacha huku tunaona ni kama jana tu umeondoka maana umeenda kimwili lakini kiroho bado tupo nawe, na kamwe hatutaacha kukumbuka malezi yako bora!
Tukiwa kama familia (watoto wako pamoja na mumeo (baba)) daima hatuishi kukuombea DUA njema kila kukicha upate kupumzika kwa kwa amani huko uliko.
Ni matumaini yetu mungu anasikia dua zetu MAMA
Ni sis wanao wapendwa Mariam, Hussein, Salum, Mariam Hawa pamoja na Baba yetu (mumeo) Sheikh Suleiman haatuna la zaidi ila ni dua tunakuombea
INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAAJIUN.

No comments:

Post a Comment