14/05/2012

Tafakuri ya Mbumbumbu





Na Emmanuely Deodath
 
Siwachukii CCM kwa sababu ya rangi za vitenge vyao na kamwe sintowapenda CHADEMA
kwa sababu ya magwanda yao ya khaki!

Kidumu Chama Cha Mapinduziiiiii…..! japo sijaweza kujua hiki chama ni cha mapinduzi yepi!
Kweli chama kikadumu…kimedumu kwa muda sasa! mpaka juzi juzi kilipoanza kudumaa. Chama
hakikudumu kwa mda wote huu eti kwa sababu mwenyikiti alisema chama kidumu nasi kuitika
kidumuuuuu….. kilidumu kwa sababu mwanzoni kilijengwa katika misingi ya mambo
yaliyodumu.
Halafu enzi hizo naona kama walikuwa hawavai sana vitenge vya kijani..au inawezekana
walikuwa wakivivaa ila tatizo ni picha zilikuwa za “black and white”, anyways….hoja si walivaa
nini, la hasha…hoja ni kwamba walifanya nini na kwa nani..unaona eeh! Chama chini ya
Mwalimu kilikataa kuburuzwa na Mabwanyeye, mabwanyenye wa ndani na wa nje, chama
kikataa viongozi kujilimbikizia mali na wakatekeleza kwa vitendo! Mfanyakazi wa umma
aliruhusiwa kulipwa kwa kazi moja tu! Hiyo ya pili na ya tatu zilikuwa ni za kujitolea kwa ajili ya
ujenzi wa taifa. Vipi leo? Mambo yakoje….na ndo maana nakichukia hiki chama, dili zinapigwa
kuanzia kwa mkuu wa kaya mpaka kwa wanazuoni….
Chama kilimilikishwa kwa wakulima na wafanyakazi, wafanyabiasiasa hawakuawa na nafasi.
Akina mzee Kaduma wanatuambia ulikuwa ukiitwa na Mwalimu unajipanga kisawasawa! Kwa
sababu Mwalimu hakuwa na mzaha ati! leo hii Doctor akikuita unaweza hata ukamvungia tu!
Hana noma…Kwa nini lakini? Doctor si mkubwa kuliko Mwalimu, au? Anyways huu ndiyo
uliokuwa mfumo wa uongozi, hakukuwa na utawala….leo hii hakuna uongozi kuna bora utawala
bora…..
Sasa wamekuja jamaa wa pipoooozzz..pawaaaa! hawa jamaa sijui wanasema chama ni mali ya
nani? Sijawahi kujua walau…wamejijenga katika misingi gani… Kwa mtizamo wangu wamejenga
chama katika hasira za wakulima na wafanyakazi dhidi ya CHICHIEM! Mimi huwa nikiwaonaga
hawa jamaa na yale magwanda yao huwa napagawa naona kama nimemwona Cheguavara!
Nasema hata waweke JIWE na CHICHIEM waweke mgombea mtu..ntalipigia JIWE LA
KHAKI…Lakini najiuliza, tayari katika mfumo wa uongozi wa chama na uwakilishi, ndani ya
CHADEMA kuna MAJIWE mangapi?? Nini mtizamo na mipango yao ya baadae endapo CCM
itapotea katika ramani na hatutakuwa na wakumchukia tena?? Au wanampango wa kuwa
wapinzani milele?? Ndani ya chama hiki nani tumtumainie…? Maana dah! Au ni Yule mzee Baba
paroko wa zamani asiye na hisa katika hii kampuni….sorry chama? Mapenzi yangu kwa hiki
chama si mapenzi ya upofu..ni mapenzi yanayoona..yanapoona kizuri yanapongeza na kibaya
kinapotokea nakemeaaa! Tusiwe na hasira kiasi cha kuchagua MAWE..walau basi ukilichagua lioombee lipate upako ligeuke kuwa MTU! Sijui kama umenisoma??? Japokuwa kwa sasa ni
ukweli ulio wazi kuwa CHADEMA ndiyo mbadala pekee wa CHICHIEM.

3 comments:

 1. Word for thought!!!
  nyanza masanja

  ReplyDelete
 2. Siasa ni sehemu ya maisha..Vyama vya siasa ni sehemu ya kuendeleza siasa..bali utawala si lazima uambatane na siasa..Uongozi ndio kabisaaaa, wala hauna undugu na siasa..uongozi unaendana na utendaji..hivyo wananji lazima waelewe nini wanataka..kati ya siasa, vyama vya siasa, utawala, na uongozi..kimoja tu kati ya hayo ndo kitawanasua na kudumaa kimwili na kiakili, kiuchumi na kifalsafa, n.k n.k

  ReplyDelete
 3. dah nimewapata "vijana wa kisasa" ninachofurahi ni kwamba mnajiuliza maswali na kuyajibu wenyewe.....sawa sisi kazi yetu ni kusoma....ila mi naomba nitoe 'mdokezo'...hivi itakuwaje pale ambapo majibu mliyotoa kwenye maswali yenu yakawa si sahihi??.....au swali lenyewe likawa si sahihi....hahaha anyway as one said "word for thought!!!...

  ReplyDelete