18/04/2013

Kutoka "Mjengoni":Yaliyokusanywa na Mwanazuoni


Yameandikwa mengi kuhusu hali ya ukosefu wa staha na heshima na matumizi ya maneno ya kukera inayoendelea kwa baadhi ya wabunge katika vikao vinavyoendelea bungeni ("Mjengoni") Dodoma. Mwanazuoni Machunde Mauma amejaribu kupitia vyanzo mbalimbali vya habari na kukusanya hatimaye kuorodhesha baadhi ya nukuu ya maneno ya kukera  zinazotumiwa na baadhi ya wabunge hao....

1. ‘‘Kuna wabunge ambao wana mimba sizizotarajiwa bungeni...”
-Mbunge wa Mtera (CCM),Livingstone Lusinde
  
2. "Sugu naomba unyamaze. Mimi ndiye nazungumza. Mimi siongei na mbwa,naongea na 
mwenye mbwa"
-Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM),Juma Nkamia

3.“UDOM (Chuo Kikuu cha Dodoma) kuna udini wa hali ya juu, wanafunzi wa dini tofauti hawalali chumba kimoja.”
-Mbunge wa Rombo (CHADEMA),Joseph Selasini

4."Kwa kuwa wanaume wengi wanabaka, kifunguliwe kituo wafundishwe kutongoza.”
-Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Leticia Nyerere

5.“Serikali iruhusu raia wa Tanzania walime bangi wapate fedha za kigeni.”
-Mbunge wa Nkasi (CCM), Ally Kesi

6.‘‘Mambo mengi nchi hii hayaendi kutokana na serikali pumbavu, hatuwezi kuwa na waziri wa elimu boya...”
-Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi

7. "Siwezi kuikubali taarifa hiyo. Nadhani huyu mtu bado amechanganyikiwa na uchaguzi wa kenya. Mimi sijaitaja Chadema bali nimesema kuna chama kimoja cha siasa, SIJUI YEYE ANAWASHWA NINI..!!
-Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde

8. "Serikali ina tatizo kwa kuwa kuna akili ndogo inatawala vichwa vikubwa.”
-Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA),Mchungaji Peter Msingwa

9. "Mbowe kaja hapa anajambajamba tu" ..."Wewe Msigwa ni mchungaji wa watu au mchungaji wa nguruwe?
-Mbunge wa Konde (CUF), Khatibu Saidi Haji

10. "Wanaume wanapoongea,watoto wa kiume wakae chini"
-Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) Mwigulu NchembaKama hali hii imefikia hapa kwa mhimili huu muhimu wa dola ni dhahiri kuwa tunakoelekea si kwema asilani! 

No comments:

Post a Comment