Utafiti uliofanywa na Mpango wa Utafiti na elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET), umeonesha kuwa idadi kubwa ya wananchi waliohojiwa wanaridhishwa na utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete huku baraza lake la mawaziri likizidi kukosa imani kwa wananchi.
Wakati chanzo cha habari hii (waweza kukifahamu kwa kubofya hapa) kikiripoti namna hii, chanzo kingine kikiripoti habari hiyo hiyo ya REDET kinasema kuwa UMAARUFU wa Rais Jakaya Kikwete unaonyesha kuendelea kuporomoka.
Chanzo hiki kinaendelea kuripoti kuwa ripoti ya REDET pia inaonyesha kuwa utendaji kazi wa Rais Kikwete, ambaye aliingia madarakani mwaka 2005 kuongoza serikali ya awamu ya nne, umeshuka kwa asilimia 28 mwaka jana ukilinganisha na matokeo ya utafiti ya mwaka 2006.
Pamoja na kushuka kwa asilimia hiyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi waliohojiwa wanaridhika zaidi na utendaji wa Rais Kikwete, kuliko wanavyoridhishwa na utendaji kazi wa baraza lake la mawaziri ambalo utendaji wake umekubaliwa na asilimia 18 tu.
Kwa mujibu wa utafiti huo, watu wanaoridhika sana na utendaji kazi wa Kikwete ni asilimia 39.5 tu kulinganisha na asilimia 69 iliyoonyesha kuridhika naye sana mwaka 2006.
Kwa undani wa habari hii kutoka chanzo hiki, waweza kubofya hapa
Wadau mna lipi la kusema kuhusiana na ripoti hii ya REDET pamoja na utendaji kazi wa Rais wetu?
nimepita kukusalimia baada kukuta kwa dada Yasinta Ngonyani, nimefurahi kuona waungwana mnazidi kuongezekana na kuijuza dunia.
ReplyDeletekaribu sana nyasa, karibu sana
Kaka Mpangala!
ReplyDeleteKumbe hujalala!
Nami sijalala!
Na wala sitalala!
Nimefurahi sana!
Kukaribishwa sana!
Nyasa si mbali sana!
Nitakuja sana!
Safari kuifupisha!
Nyasa kunikaribisha!
Link nimeimuvuzisha!
Kulia imejipumzisha!
Tuendeleze libeneke!
Mpaka kieleweke!
Ukweli tuuweke!
Nyumba tuiezeke!
propaganda labda zina utamu wake pia
ReplyDeleteKaka Mwanasosholojia unazidi kunishangaza kila siku. Sikujua kama ni makini kwa mashairi.
ReplyDeleteNajaribu Yasinta dadangu!
ReplyDeleteMashairi burudani yangu!
Yanipa amani moyoni mwangu!
Nayatumia kwa nchi yangu!
Nami nakubali,
ReplyDeleteNi kweli burudani,
Nami mwangu moyoni,
Napata raha kweli,