Alhamisi ya wiki hii hapa University College Dublin (UCD), Ireland ilifanyika warsha iliyoambatana na uwasilishwaji wa mada zinazohusu utafiti katika nyanja ya maendeleo. Warsha hiyo iliyoandaliwa na Programme of Strategic Co-operation between Irish Aid and Higher Education and Research Institutes, ililenga kutambulisha kazi za kitafiti zinazofanywa na wanafunzi wa shahada ya uzamivu (PhD in Global Human Development). Nchi ya Ireland kupitia taasisi ya Irish Aid pamoja na Higher Education Authority inadhamini masomo ya jumla ya wabongo kumi kutoka University of Dar es Salaam, ikishirikiana na chuo hiki. Kwa ujumla wabongo hawa waliwakilisha vyema nchi yetu katika warsha hiyo na kwa kiasi kikubwa kuwaonesha wazungu (siku hizi wanapenda kuitwa partners in development), kuwa si haba katika kutumia utafiti kama njia ya kutoa matokeo yatakayoongeza mchango wa elimu katika kutatua matatizo mbali mbali ya jamii. Waweza kujipatia angalau kwa uchache wake, taswira za siku hiyo ya warsha hapa chini;
Mdau Lupa Ramadhani kutoka bongo akisisitiza jambo alipokuwa akiwasilisha mada
Mdau Engineer George Lupakisyo Mwalwiba kutoka bongo akiwasilisha mada yake
Mmoja wa watoa mada, Michelle D'Arcy kutoka UCD.
nawashukuru hao wadau kwa kutuwakirisha inaletesha moyo na inapendeza kuona hawakuwa/hatupo nyuma.
ReplyDeleteSaaafi sana. Nina uhakika wako wengi na mahala pengi wakifanya mema mengi lakini hawaonwi na wengi.
ReplyDeleteAsante kwa kuwaona, kuwatambua na kuwawakilishia kazi zao nzuri hapa
Baraka kwenu
Mzee nimekubali, unajua tatizo ni kwamba si rahisi kujua nani yu wapi na anafanya nini. Nafikiri kwa jitihada kama hizi wengi tutawaona na kujua wanafanya nini na hatimaye kuhamasisha wengi ambao wanahitaji kutiwa moyo ili wafanye makubwa zaidi.Big up bro,na wengine toka nchi nyingine watuonyeshe pindi wanapoitoa bongo kimasomaso.
ReplyDelete