14/09/2009

Kushikiwa bango Kanumba na Ung'eng'e Bongo

Msanii Steven Charles Kanumba

Kwanza napenda kuwataka radhi wadau kwa kimya cha Mwanasosholojia cha takribani miezi miwili. Nilikuwa huko ndani ndani wanakoishi ndugu zangu wadanganyika wenye nia, ambako teknolojia kama hii wanaisikia kwa "bomba" tu.

Baada ya kurudi jijini na kujipanga kuweka kimaandishi nilichokifuata huko udanganyikani, leo nimeona vyema kurudi barazani. Nimefurahishwa na mjadala uliovuma hivi punde juu ya uwezo wa wabongo, hususani wasanii wetu katika kutema ung'eng'e, hasa kufuatia mgeni mwalikwa katika jumba la "Bigibraza", msanii mwigizaji na mwimbaji Steven Kanumba kudaiwa "kuchemsha" katika kubonga ung'eng'e ndani ya jumba hilo.

Si tu vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti suala hili, bali hata wengi wetu tumepokea ujumbe kwa mfupi wa maneno katika simu zetu za viganjani, pengine ukiwa umeongezwa chumvi kwa njia ya kuchekesha (na hata wengine wanasema kudhalilisha) ukielezea jinsi mbongo mwenzetu Kanumba alivyokuwa anachapia kimombo jumbani.

Hapa kuna masuala kadhaa ya kujiuliza, kwa upande mmoja sisi kama watanzania tunapigia upatu Kiswahili kama lugha ya Taifa, na hata kuanza kufanya jitihada za kukitumia katika mikutano mbalimbali (nakumbuka hotuba za viongozi wetu wa juu katika mikutano ya Umoja wa Afrika), lakini kwa upande mwingine lugha ya kiingereza inaendelea kupeta kama lugha ya kimataifa inayotumika katika maeneo mengi.

Ukinzani huu wa ukweli unamlazimisha Mwanasosholojia kutamka kwamba tunapaswa kutukuza utamaduni wetu na kuweka mkazo katika kukuza lugha yetu ya Kiswahili, bila ya kuona aibu kwa wenzetu kwa nini tunatumia Kiswahili. Kutamka hivi kunatokana na ukweli kwamba, kama tunaogopa aibu kwa kuchapia kutumia lugha ya wenzetu tunaweza kufanya mambo mawili; kwanza ni kukomaa kuongea lugha yetu na inapobidi atafutwe mkalimani, pili kama tunaona aibu basi tujifungie na kujifunza kwa bidii huo ung'eng'e ili kutochapia na kuizoa aibu hata miongoni mwetu.

Mgeni anayetumia kimombo kwa mfano akiongea kiswahili cha kuchapia mara nyingi hadhihakiwi, zaidi huelekezwa usanifu wa lugha anayotumia, lakini mswahili akiongea kimombo cha kuchapia huchekwa na hata waswahili wenzake! Hii ni kasumba ambayo imejijenga kwa miongo mingi. Kama Mwanasosholojia alivyoweka bayana awali, hatuna haja ya kuendelea kuchekana na kudhihakiana wakati tuna lugha yetu inapotokea tunajiona hatuna uwezo wa kutumia lugha ya wenzetu. Inashangaza kuona mtu anakomaa kuchapia lugha ye wenzetu wakati anaijua fika ya kwake, labda ni kule kuona aibu kuwa utaonekana hujui kimombo, kwani kimbo si ni lugha tu pamoja na kwamba inakingiwa kifua kimataifa... huu ni utumwa wa kifikra ambao si vyema ukaendelea.

Mjadala huu wa Kanumba ulimpelekea Mwanasosholojia kutafuta undani wa msanii huyu. Yeye anamiliki tovuti, ukiipitia hata tovuti yake unagundua kuwa anatumia King'eng'e "chenye matege", jambo ambalo alipaswa kuliangalia kwa kuamua tu kutumia Kiswahili au kama alitaka aonekane wa kimataifa basi alichoandika alipaswa kumpatia mhariri mwenye ufahamu wa kimombo kilichonyooka, kabla ya kukitundika tovutini. Labda wadau nanyi mpate fursa ya kusoma angalau wasifu wa Msanii Kanumba aliouandika kwa kin'geng'e na kuupachika kwenye tovuti yake;

Steven Charles Kanumba is my name, i was born in a Christian family of 2 girls and i happen to be the last born and the only boy to Mr. & Mrs. Charles Meshark Kanumba. I was given birth on january 8th 1984. I originate from Shinyanga region in Tanzania. I am Sukuma by Tribe. I completed my Primary Education in Bugoyi Primary School in Shinyanga. After Completing my primary education i started my secondary education right away in Mwadui Seminary Secondary School in shinyanga where by i shifted to Dar-es-salaam Christian Seminary Secondary school here in Dar-es-salaam when i was still in form II and complete my O-Level Education there. Thereafter i moved to Jitegemee Sec. School to complete my A. Level Education.

Growing up, acting has always been something that i really liked to do. Apart from that i also liked singing and that made me grave to be an artist while i was still in teens, still in school ie. i started acting in church a lot of people told me i had a talent so i decided to join Kaole Sanaa Group which delt with Acting. After joining Kaole Sanaa Group i met different Teachers from Bagamoyo and other College who helped me to build up my career of Acting for a period of 1 year, after that i got a special Training from University of Dar es salaam Under Doctor Nyoni for about 3 months therefore i was sure to go to work and indulge myself in Soap Operas/Series. i then took acting as my career. Little by little i got to win peoples' attention which made me work even harder and become successful.

After all the hard work that i kept in series i decided to play a part in movies so i took a step forward and associate myself in film industry. i happen to do a lot of movies that did very well in the market and i'm still doing movies up today and it just get better day by day. in addition to this i archieved a lot through my hard work that is prestigious awards, travel across different countries, working with people from different part of the world meeting different people and learn new things and experiencing different life.

I also got to get to work with Nollywood in Nigeria where by i did more than five movies with famous actors from Nolllywood, it was the wonderfull experience. I also got a chance to Visit The United States of America and there is where i got the experience of a lifetime i got visit Hollywood, Warner Bros Pictures, Universal Studios and Disney Land, i learnt a lot i met people who work there so i got to ask alot of Quaestions and gained a lot of knowledge.

Speaking about me as Steven Kanumba i'm a very down to earthguy i like hanging out with my friends and i like to associates myself with people, i love children with all my life, i'm just a simple guy, i'm not outgoing a lot, i love going to movies and just be chilled out and relaxed places. I'm not married for the time being but i am in a commitment in the name of God i hope that one day we will get married.

I would like to end with my most sincerly appreciation, first and foremost i would like to thank God Almighty for giving and Blessing me a beautiful talent cause apart from acting being my Job, it also happen to be something i love doing and when i am at it i do it with passion. I would also like to thank my whole family but special appreciation goes to the most beautiful woman in the whole world that happened to be my mother (I Love you Mom) would also like to thank Game 1st Quality Tanzania Limited and again special thank to my brother, my executive Producer and my Advicer Mr. Mtitu G. Game and His Wife. I Would like to thank all the Artist, Producers and Directors i have worked with. Also my special Thanks to my sister Sharifa Kalala in USA and Sanura Hussein in Denmark. Most Importantly, i would lastly like to thank all my fans from different part of the world, thank you all very much for supporting me, I LOVE YOU all and God bless you.

Wadau mwaweza kumtembelea msanii wetu Kanumba tovutini kwake kupitia http://www.kanumba.com




9 comments:

  1. Nafurahi kuwa umerudi na kuwa nasi binafsi niliku-miss.

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana dada yangu
    Nimerudi ukumbini kwangu
    Niliwamiss wadau wangu
    Ukiwemo Yasinta ndugu yangu

    ReplyDelete
  3. Nafikiri Watanzania tuna bomba la inferiority complex kinamna kitu kitufanyacho tusijiamini hata kwa tuliyosahihi!:-(

    Mimi naamini ni rahisi kabisa kwa Watanzania kukubali kuongozwa hata kwa mambo wanayoongoza kwa kufikiri kuwa kwa yetu ndiko kwenye mapungufu hasa tukiwa tunadili na wageni.

    Na katika lugha unaweza kuliona sana hata vijijini. Ingawa katika vijiji KWA UZOEFU WANGU mara nyingi ni asiyeshuka vizuri kiswahili na mgeni kutoka mjini ndio achekwaye!:-(


    Kwa uzoefu wangu binafsi tena,.... mimi Baba yangu ni Mpare na Mama ni Mjita na kote Upareni na Ujitani hakuna nilikokuwa nakosolewa kwa kuwa lugha zote hizo mbili kwangu hazipandi vizuri na kwa kawaida ni wao niliowakuta huko vijijini nikienda kuwatembelea ndio wanachekana wakikosea kuongea na mimi kiswahili lakini wanaona ni kawaida nikikosea na huwa haswa nakosea.


    Kwa kifupi nachotaka kusema ,.... NAHISI sababu kubwa ya Tanzania kutawaliwa na Wakoloni na mpaka kujikuta tumebadilishwa mpaka dini , siamini ilikuwa ni silaha za wageni zilizotubadili , bali ni kutojiamini na ya kwetu!


    NI wazo tu!:-(

    ReplyDelete
  4. THERES NOTHING SO SPECIAL, JUST BLAHBLAH.
    BIG UP BR.
    Debby.

    ReplyDelete
  5. Karibu tena. Mimi nawashangaa wanaopiga kelele, jaribu kuwaambia wao waongee kiswahili, utashangaa wana kiswahili kibovu kwelikweli, na wakati mwingine sijui wwanaongea lugha gani sijui, maana kiingereza si kiingereza na wala si kiswahili, ni mseto wa maneno tu.

    ReplyDelete
  6. Jamani kaka yetu karibu sana nimefurahi sana umerudi.Tulikumis sana.Hii ya Kanumba kazi kweli kweli,ushauri wangu aende english course sio kwa ubaya wala nini.Tupo pamoja kaka.

    ReplyDelete
  7. Ahsante kaka Kitururu, Debby, Chib na dada yangu Manka nawashukuru sana!

    ReplyDelete
  8. pengine wakasoaji walikuwa wanamkosoa mtu asiye sahihi kukosolewa. Nikuchukua mfano wa Kitururu hapo juu kuwa akienda vijijini kwao alikuwa hachekwi kwa kuwa walijua kuwa hajui vema viluga vya huko. shida katika hili la kanumba ni kumpeleka mtu asiyestahili. madongo yalitakiwa yaende kwa multichoice, sio kanumba. hapa tunakubaliana kanumba hajui kizungu vema, which is not a curse. the sama kitururu asivyojua kipare na jijita is not a curse. kama kulikuwa na ujumbe wa kupeleka upareni na huko hakuna lugha nyingine mbali na kipare, sidhani kama kitururu angeteuliwa kwenda huko. ujumbe katika big brother ni kwa kizungu. kama ilikuwa lazima mtanzania atuwakilishe, kanumba hakustahili. kutojua kizungu kwake is not a curse, lakini kupelekwa kwake mule jengoni kulikuwa na maana tu ya yeye kwenda 'kuongea' na washiriki ili kuwakaribisha na kuwatoa hofu. sasa utaongea nao nini kama kizungu chako ni kama cha kwangu. ila multichoice kama wana akili ujumbe ulikuwa kwao sio kwa kanumba.

    pia napinga kuwa kanumba katuzalilisha. hapana. kila asiye mtanzania anajua watanzania hatubongi kizungu vema. that is what they expected.

    ReplyDelete
  9. Kuna ukweli katika uyasemayo John. Hata mikutanoni kama sio nguli katika lugha ya kiingereza hutafutwa mkalimani!

    ReplyDelete