26/03/2009

Leo Kumbukizi ya Jabali Marijani Rajabu

Marijani enzi za utoto (Picha kwa hisani ya Mkuu wa Wilaya ya nanii, Issa Michuzi na Blogu ya Jamii)

Imeshatimu miaka 14 tangu "Jabali la Muziki Tanzania" Marijani Rajabu atangulie mbele ya haki. Nafikiri wadau mnakumbuka nyimbo zake nyingi zenye mafunzo ambazo zinaendelea kutamba hadi leo. Kuna kitu cha kujifunza hapa; Ipo haja ya kumuenzi Jabali huyu ili kazi zake ziendelee kudumu kati ya vizazi na vizazi, lakini pia ipo haja ya kufanya juhudi za kuibua vipaji miongoni mwa vijana ili tuendelee kuwa na majabali wengine kama Marijani.


Nadhani wadau mnakumbuka hata zile tungo zake za mahusiano zilivyokuwa zimepangiliwa kimantiki. Mfano ile tungo ya Georgina akiwa na Safari Trippers, hebu onja kidogo;


Ooo Georginaaaa.... Siku uliyoondoka, uliniacha nalia na machozi. Umekwenda kuishi mbali nami, Georgina wa mamaaaa.Sipati usingizi, nikikumbuka tulivyoishi mimi nawe Georginaaaaa.Ooo Georgina. (Rudia)

(Kiitikio)Umeondoka Georgina, umeniachia masikitikoGeorgina, Georgina oooo (Rudia)

[Marijani]Nauliza Georgina oooo...Ni lini utarudi? oooooo...Uniondoe wasiwasi... ooooooooGeorgina wa mama aaa....Georgina Georgina oooo(Rudia)...

Waweza kujisikilizia tungo zenye mafundisho za Jabali huyu kama vile Dunia Uwanja wa Fujo na Ndoa za Mateso kwa kubofya;


No comments:

Post a Comment