28/04/2009

REDET Wamsafishia Njia JK

Rais wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete

Utafiti uliofanywa na Mpango wa Utafiti na elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET), umeonesha kuwa idadi kubwa ya wananchi waliohojiwa  wanaridhishwa na utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete huku baraza lake la mawaziri likizidi kukosa imani kwa wananchi.

Mwenyekiti mwenza wa REDET Dr Bernadetha Killian amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanyika novemba mwaka jana na kuhusisha mikoa yote 26, zaidi ya asilimia 78.6 wameeleza kuridhishwa na utendaji wa rais Kikwete, ikilinganishwa na asilimia 67 kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2006.

Dr Killian amesema licha ya wananchi kuwa na imani na rais wao, bado utafiti umeonyesha kuwa wananchi hawana imani na baraza la mawaziri, kutokana na kutokuwa makini katika utendaji kazi wao.

Amezitaja sababu zilizotajwa na waliodai kutoridhika na utendaji wa mawaziri kuwa ni pamoja na kushindwa kusimamia utekelezaji wa ahadi ya serikali ya kuboresha hali ya maisha,pamoja na kushindwa katika vita dhidi ya rushwa na vitendo vya kifisadi, kushindwa kutatua kikamilifu tatizo la madai ya walimu na madai ya wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu nchini

Tathmini ya utendaji kazi wa serikali na baadhi ya taasisi zake, ripoti ya REDET imeonesha kuwa, Bunge limeonesha imani kubwa zaidi kwa wananchi, huku taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU ikiendelea kupoteza imani yake kwa wananchi.

Taarifa ya  REDET imebainisha kuwa, utafiti huu hii ni changamoto kwa serikali iliyopo madarakani kujipanga upya kutokana na wananchi wengi kutokuwa na imani na baraza la mawaziri.

Wakati chanzo cha habari hii (waweza kukifahamu kwa kubofya hapa) kikiripoti namna hii, chanzo kingine kikiripoti habari hiyo hiyo ya REDET kinasema kuwa UMAARUFU wa Rais Jakaya Kikwete unaonyesha kuendelea kuporomoka.

Chanzo hiki kinaendelea kuripoti kuwa ripoti ya REDET pia inaonyesha kuwa utendaji kazi wa Rais Kikwete, ambaye aliingia madarakani mwaka 2005 kuongoza serikali ya awamu ya nne, umeshuka kwa asilimia 28 mwaka jana ukilinganisha na matokeo ya utafiti ya mwaka 2006.

Pamoja na kushuka kwa asilimia hiyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi waliohojiwa wanaridhika zaidi na utendaji wa Rais Kikwete, kuliko wanavyoridhishwa na utendaji kazi wa baraza lake la mawaziri ambalo utendaji wake umekubaliwa na asilimia 18 tu.

Kwa mujibu wa utafiti huo, watu wanaoridhika sana na utendaji kazi wa Kikwete ni asilimia 39.5 tu kulinganisha na asilimia 69 iliyoonyesha kuridhika naye sana mwaka 2006.

Kwa undani wa habari hii kutoka chanzo hiki, waweza kubofya hapa

Wadau mna lipi la kusema kuhusiana na ripoti hii ya REDET pamoja na utendaji kazi wa Rais wetu?

6 comments:

  1. nimepita kukusalimia baada kukuta kwa dada Yasinta Ngonyani, nimefurahi kuona waungwana mnazidi kuongezekana na kuijuza dunia.
    karibu sana nyasa, karibu sana

    ReplyDelete
  2. Kaka Mpangala!
    Kumbe hujalala!
    Nami sijalala!
    Na wala sitalala!

    Nimefurahi sana!
    Kukaribishwa sana!
    Nyasa si mbali sana!
    Nitakuja sana!

    Safari kuifupisha!
    Nyasa kunikaribisha!
    Link nimeimuvuzisha!
    Kulia imejipumzisha!

    Tuendeleze libeneke!
    Mpaka kieleweke!
    Ukweli tuuweke!
    Nyumba tuiezeke!

    ReplyDelete
  3. Kaka Mwanasosholojia unazidi kunishangaza kila siku. Sikujua kama ni makini kwa mashairi.

    ReplyDelete
  4. Najaribu Yasinta dadangu!
    Mashairi burudani yangu!
    Yanipa amani moyoni mwangu!
    Nayatumia kwa nchi yangu!

    ReplyDelete
  5. Nami nakubali,
    Ni kweli burudani,
    Nami mwangu moyoni,
    Napata raha kweli,

    ReplyDelete