15/04/2009

Taswira katika Tamasha la Wasomi wa Nyerere, UDSM

Maprofesa wakisikiliza maswali na maoni ya washiriki. Kutoka kushoto ni Prof. Wole Soyinka kutoka Nigeria, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala na Mhadhiri Mstaafu na Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, UDSM, Prof. Issa Shivji.

Wasomi na wanazuoni wakimsikiliza Prof. Wole Soyinka alipokuwa akitoa mhadhara wake.


Mwanaharakati wa Nigeria, Profesa Wole Soyinka,akizungumza na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na nje ya chuo hicho Aprili 13 2009 katika Tamasha la Kwanza la Kimataifa la Wasomi wa Nyerere (Picha zote ni kwa hisani ya Mdau wangu, Kamarade, Mroki Mroki "Father Kidevu")


1 comment:

  1. Kongamano kama hili linaamsha hisia za uzalendo kwa walio wengi. Huu ni mwanzo, ni vema kongamano hili likifanyika kila mwaka. Mimi nimejifunza kitu kimoja kwamba, wakati watazania wanayatia kapuni mawazo ya Mwl. JK Nyerere, wenzetu duniani wanaona hiyo ni hazina inayofaa kuenziwa. Je, nani wa kutuamsha?

    ReplyDelete