31/05/2009

Mwanasosholojia Ndani ya Bongo!

Moja ya mandhari ya jiji la Bongo

Wadau wangu kwanza naomba mnisamehe sana kwa kutowarushia mpya zozote katika kipindi hiki cha siku takribani sita tangu niwasili Bongo Jumatatu usiku. Natumaini nimesamehewa.

Mwanasosholojia aliingia Bongo salama usalimini na kulakiwa na familia, rafiki, ndugu na jamaa zake. Aliona raha sana kuwakuta wote wakiwa salama usalimini, na zaidi kupewa michapo ya jiji la Lukuvi (si jiji la Kandoro tena siku hizi ati!). Jumanne Mwanasosholojia alikwenda kusabahi wazazi wake wanaoishi kitongoji kimoja pembeni kidogo ya jiji la Lukuvi. Aliwakuta salama, na alifurahi pia kumuona mama yake ambaye alipata kufanyiwa upasuaji baada ya kupata matatizo ya utumbo kujikunja (kwa kidhungu intestinal obstruction) miezi miwili ilopita.

Kama ilivyo kawaida, Mwanasosholojia alikaribishwa Bongo kimtindo pia, kwa kukumbushwa kuwa asijisahau na jiji hili baada ya kuibiwa vioo viwili (side mirrors) vya gari (si lake, aliazima!). Tukio hilo lilitokea hapa hapa chuo kikuu cha Dar es salaam sehemu ya Mlimani, akiwa amepaki eneo la Hill Park. Alilazimika kununua vioo vingine kwa ajili ya kurudishia. Hii ilimkumbusha Mwanasosholojia kuwa, amerudi Bongo na anapaswa kuwa makini, chochote unachotumia au kushika barabarani, si mali yako ati...kina wenyewe, wakiamua wanaweza kukichukua muda wowote! Ndo Bongo hiyo!

Sasa Mwanasosholojia yupo ndani ya Bongo, ingawa mtandao si mzuri kama ilivyokuwa Dublin, anaahidi kuendeleza libeneke hili mpaka kieleweke. Wadau endeleeni kumpa moyo na kumuunga mkono, bila ninyi libeneke hili haliwezi kusimama!

7 comments:

 1. Mmh! Bongo natamani ningekuwa nawe huko Bongo Nyumbani ni nyumbani. Jitahidi kula vyakula fresch huko. Pole kwa kuibiwa kweli inabidi uwe makini.Namshukuru Muumba umesafiri salama na pia umekuta familia yako wazima. Mpe pole na msalimie mama.

  ReplyDelete
 2. Tunamshukuru Mungu ulifika salama,na pia kuikuta familia wazima. pole sana kwa kuibiwa vioo vya gari,Usijisahau hiyo ndio bongo yetu unatakiwa uwe makini sana.Tupo pamoja.

  ReplyDelete
 3. Dada zangu Yasinta na Manka, nawashukuru sana! Ahsanteni kwa pole zenu, nitajitahidi kuwa makini! Tuendelee na libeneke letu!

  ReplyDelete
 4. Mwanasosholojia,

  Hongera sana kwa kufika salama, naamini utapata muda mzuri kutembelea sehemu zote za jiji la Lukuvi, Nimekumbuka sana hapo Kariakoo,m Manzese na jua kali la Buguruni.

  Likizo njema

  ReplyDelete
 5. Habari njema,Mwanasosholojia,kuwa umefika salama na "bimkubwa" hajambo baada ya upasuaji.Tunategemea kupata michapo zaidi kutoka huko nyumbani,ila kuwa makini na vibaka.Ni kama wana nyenzo zaidi za kutambua wageni,maana hata mie niliwahi kulambwa simu siku ya pili tu baada ya kutia mguu huko.
  Baadhi ya wenye kumiliki biashara ya mtandao ni wahuni (au tuwaite mafisadi) kwani wanafurahi kuona kasi ya mtandao ikiwa ya chini kwa vile inawanufaisha:ili usome emails kadhaa na kzijibu,na kuweka mabandiko kwenye blogu basi kwa spidi ya 50-100 kb/s wa uhakika wa shilingi alfu kadhaa.

  Kila la kheri Mwanasosholojia.

  ReplyDelete
 6. Ahsante sana Evarist! Ni kweli, pole na wewe, mtandao ndo tunakwenda nao hivyo hivyo!Bongo Dar es Salaam!

  ReplyDelete
 7. Karibu Bongo, gurudumu la maendeleo linategemea pia ujuzi na maarifa yako

  ReplyDelete