18/05/2009

Tunamjongea zaidi Mungu kwenye vipindi vigumu tu?- 2

Wadau, Jumapili hii tena nimepata taarifa kutoka kanisani (mi sikwenda, nilibana homu ingawa nilipata wasaa wa kumwomba Saa Godi), rafiki yangu Muitaliano aliyekwenda chachi ameniambia kuwa ameshangaa sana kukuta chachi ambalo lilifurika jumapili ile ya tarehe 10 (wakati wanafunzi wakiwa kwenye mitihani), jumapili hii siti nyingi za chachi zilikuwa tupu. Anasema kwa kifupi kanisa lilikuwa limepwaya ile mbaya, kondoo wa bwana wachacheeeee, mpaka mchunga kondoo akahoji kulikoni?. Sasa hii ndo kusema ile nadharia ya kumjongea Mungu kwenye vipindi vigumu na wakati wa shida tu ina ka- ukweli?


Taswira ya chachi linapokuwa limefurika kondoo wa bwana, hapa inaonekana kila mmoja anajitahidi kumkonvisi Saa Godi asikilize shida au mahitaji yake...

Na hapa taswira nyingine ya chachi likiwa na kondoo wachache tu...benchi nyingine zikiwa tupu, inaonesha kondoo wengine wamesepa...

No comments:

Post a Comment