10/06/2009

Mwanasosholojia Jr Azaliwa!

Jamani wadau wangu, sina budi kushea nanyi furaha niliyo nayo leo! Mimi na mama Mwanasosholojia tumepata mtoto wa kiume usiku wa kuamkia leo. Kwa muda tunamwita Mwanasosholojia Jr. wakati tunafikiria jina la kumpatia. Natamani mtoto huyu aje kuwa Mwanasosholojia! Huenda akaja kuwa Mwanasosholojia. Ni mtoto wetu wa tatu baada ya Agripinus mwenye umri wa miaka minane (alizaliwa tarehe ya leo, 10/06), anasoma darasa la pili na binti yetu Magreth ambaye kwa sasa ana umri wa miaka mitano, na anasoma darasa la kwanza hapa Dar es Salaam. Tunawashukuru wapendwa ndugu, rafiki na jamaa zetu ambao wamekuwa nasi bega kwa bega katika kipindi chote tulichopitia.

Nachukua nafasi hii pia kuwajulisha wadau kuwa, pamoja na kuongeza memba katika familia yangu, jana mama yangu alilazwa hospitalini baada ya hali yake kubadilika ghafla na kupata kitu kama dege dege. Tulimuwahisha kituo cha afya cha Chuo Kikuu Kampasi ya Mlimani, ambapo anaendelea kupata matibabu. Mpaka asubuhi hii hali yake ilikuwa inaendelea vizuri, pamoja na dawa nafikiri pia hasa baada ya kupewa taarifa za ujio wa Mwanasosholojia Jr. (mumewe!!!)

9 comments:

  1. Hongereni sana tena sana kwa kuongeza member na pia hongera kwa kaka mkubwa na dada Magreth.

    Na mpe pole sana mama augue pole.

    Mungu yupo nanyi. Asante ni hayo tu kwa leo.

    ReplyDelete
  2. da Yasinta ahsante sana
    Kwa kutupa hongera sana
    Kweli tuna furaha sana
    Kuongeza Memba familiani

    ReplyDelete
  3. Hongereni sana kaka yetu,tunamtakia mama na mwana afya njema.Tunamuombea mama augue pole.

    ReplyDelete
  4. Mwanasosholojia,

    Hongera sana kwa kutuongezea nmwanasosholojia mwingine kwani tunahitaji sana wanasosholojia wengi ukizingatia dunia imebadilika na upweke na mengine yanayofanana na hayo yahahitaji watu muhimu kama mgeni aliyekuja (junior).

    Pongezi kwa mke wako na wewe mwenyewe pia.

    Tunawatakia malezi bora kwa mtoto ili atimize ndoto za wazazi na yeye mwenyewe pia ila usishangae siku akiamua kurusha ndege angani badala ya kuwa mwanasosholojia.

    Hongera sana

    ReplyDelete
  5. Hongereni sana, Mungu amjalie Jr awe na afya tele na umri mrefu.
    Tram.

    ReplyDelete
  6. Hongera nyingi kwa kutuletea mwanasosholojia mwingine.

    ReplyDelete