22/09/2009

Eti hizi ni Sababu 37 za Mwanaume Kuamua Kuoa!


Hutokea mtu kujiuliza sababu hasa zinazopelekea kuamua kuoa/ kuolewa, hususani kwa wale wanaofuatilia mijadala ya ndoa, na hata wale walioamua kukata shauri kuishi maisha ya kikapera. Wachambuzi wa mambo ya mahusiano na ndoa wanasema kuwa kuna sababu zisizopungua 37 zinazopelekea mwanaume kuamua kuoa. Haiwezekani ikawa ni sababu zote, la hasha! Ila wanasema miongoni mwa hizo 37 lazima kuna ambayo/ ambazo zinapelekea uamuzi wa kuoa.

1. Kuwa na mwenzi wa maisha
2. Amempata mpenzi wa kweli
3. Ni muda muafaka kuoa
4. Umri unakimbia...anaukimbilia uzee
5. Ana nyumba kubwa na yupo peke yake
6. Ana watoto aliozaa na mke wa awali na hana msaidizi wa kuwatunza
7. Anahitaji msaidizi wa kazi za ndani wa kudumu
8. Ana pesa nyingi na muda
9. Amechoshwa na mke/ wake alionao
10. Dini inamruhusu kuoa

11. Anahitaji mtu wa kumzalia watoto
12. Mkewe wa awali ni tasa
13. Amekuwa mkubwa na anahitaji mwenye umbo la umama ili amtunze
14. Anahitaji kuridhishwa kimapenzi
15. Wazazi wake wamemlazimisha kuoa
16. Anaona wenzake wa rika moja wanamwacha nyuma kwa kuoa...anawakimbilia
17. Hawezi kupika, anakula hotelini na kwa mama ntilie...anahitaji mpishi nyumbani
18. Hawezi kusema hapana kwa kuwa mama wa mchumba wake ameshaanza kufanya maandalizi, amelipia ukumbi na kuwaarifu ndugu, jamaa na marafiki wote
19. Mchumba ni tajiri sana
20. Baba wa mchumba ni tajiri sana

21. Baba wa mchumba anafanya biashara na anayetaka kuoa
22. Anataka kumjali kwa ukaribu anayemuoa maisha yake yote
23. Mchumba anampenda sana na anaweza kufa ikiwa hatamuoa
24. Anaoa ili wazazi wake waache kupiga makelele kumuhimiza
25. Anaoa kwa kuwa wazazi wake wanamsifia mchumba wake kuwa ni mrembo
26. Anaoa kwa kuwa amempa rafikiake ujauzito
27. Anaoa kwa kuwa anaogopa kuuawa na baba wa aliyempa ujauzito
28. Anaoa ili mchumbake apate uraia
29. Anaoa kwa kuwa ni rafikake wa toka udogoni
30. Anaoa kwa kuwa mwanamke ameapa kutomwacha maishani

31. Anaoa kwa kuwa muda mrefu amekuwa akitaka kuanzisha familia
32. Anaoa ili amalizie maisha yake yaliyobaki na yeye
33. Anaoa ili apate matunzo bora kutoka kwa anayemuoa
34. Anaoa ili mwanamke aweze kutoka kwao na afaidi uhuru

35. Anaoa kwa sababu tu anafikiri anampenda sana
36. Na kwamba anafikiri anapendwa sana
37. Anaoa kwa kuwa ni lazima apitie hatua ya kuoa


Wadau wababa na wakaka; kama hujaoa, sababu zipi kati ya hizo unafikiri zitakupelekea uoe? Kama umeoa, ni zipi zimekupelekea uoe?

Wadau wamama na wadada hali kadhalika, unafikiri utaolewa kwa sababu zipi kati ya hizi, au kuna ukweli kuwa umeolewa kwa sababu yoyote kati ya hizi?

9 comments:

  1. Ni kweli kaka leo tumeamka na mawazo sawa. Haya mambo haya ni tofauti kwa kila mtu kuna wanoolewa kwa ajili ya kufuata pesa, kwa vile kijana nimrembo, au kwa vile anataka kuja katika nchi nyingine. Lakini nadhani hilo sio penzi kama watu wanafanya hivyo na naamini wapo. Mi nimeolewa kwa penzi ni hilo tu.

    ReplyDelete
  2. Nimefurahi dada yangu kutabanaisha kuwa umeolewa kwa penzi,hongera sana. Umenifanya nianze kufikiria kurusha mjadala wa mahusiano kwa wanaooa au kuolewa kwa penzi. Natumaini utatoa mchango mahususi dada yangu.

    ReplyDelete
  3. Ntajaribu kakangu kwani unajua ktk hizi blog tunafunzana mengi sana.

    ReplyDelete
  4. Kaka yangu hii ya leo kali!Ni kweli kuna wanaooa au kuolewa kupitia hizo sababu hapo juu inasikitisha sana,lakini ndio binadam tulivyo.Mimi nimeolewa kwa penzi la dhati.

    ReplyDelete
  5. Pongezi kwako Manka...maanake nilitaka kufikiri ni kwa yale mambo yetu yaleee....ya "kabati ya mbeho", teh!

    ReplyDelete
  6. Sijapita hapa siku nyingi kidogo. Kumepamba moto kweli kweli. Sababu zote nilizokuwa nazifikiria umeshazibainisha hapa. Je,inawezekana pia kuoa/kuolewa bila sababu yo yote?

    ReplyDelete
  7. Karibu sana kaka Masangu..Mmh!Kwa kweli hapo napata kigugumizi kidogo na mdomo kunijaa mate...labda wadau wengine watusaidie...

    ReplyDelete
  8. Hapo nyingi zimenikuna!

    Ila kuna ambazo kama mtu huna LIMTU, ukikiri ndio sababu ya kutaka kuoa kuna watakao toka baruti kwa mfano hiyo namba saba;ETI:

    7. Anahitaji msaidizi wa kazi za ndani wa kudumu.
    Mhh!
    Hapa ni kutafuta mke au Housegirl?

    ReplyDelete
  9. Nimecheka sana kaka kabati ya mbeho muhimu!

    ReplyDelete