25/02/2010

Mpigie Kura Mdau Makulilo Jr

Makulilo Jr.
"Mwanablogu" nguli wa kupasha habari za "skolaship" Ernest Makulilo almaarufu kama Makulilo Jr. ni mmoja wa washindani katika mashindano yajulikanayo kama DELL SOCIAL INNOVATION COMPETITION ambayo yanashindanisha dhana za mambo ya jamii (social issues ideas) ambapo mshindi atapata dola 50,000 kuweza kutimiza project yake ambayo ameelezea.
Mdau huyu anaomba wadau waweze kumpigia kura na kutoa maoni yao ambayo yatasaidia kuingia katika 10 bora na hatimaye kuinuka kidedea.
Unachotakiwa kufanya ni kufungua tovuti hii hapa chini, na kisha kujisajili ili uweze kutoa maoni yako na kupiga kura yako (Join the community to vote and comment on your favorite ideas! )

Unaweza kuona ideas za watu wengine pia hapa

Jamani wadau tumpigie upatu mdau mwenzetu. Kwa libeneke lake mtembelee kwa kubofya hapa na hapa

2 comments:

  1. KURA YANGU? atapata tu lakini avue suti ha ha ha ha ha ha

    ReplyDelete
  2. ahhahahahah Nashukuru kwa kura yako kaka Mpangala. Suti mara moja moja, nakula tizi la kuvaa suti sasahivi sababu ya kujiandaa na harusi ndugu.

    MAKULILO, Jr.

    ReplyDelete