18/02/2010

Rais Kikwete Kutunikiwa Nondozz Nyingine ya PhD

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya, Dk.Harris Mule akimtunuku Phd ya Heshima Rais Jakaya Kikwete mjini Nairobi mwaka 2008

Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya heshima na Chuo Kikuu cha Fatih cha nchini Uturuki. Hii itakuwa ni shahada ya pili ya ngazi hiyo baada ya ile aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya mwaka 2008, kutokana na jitihada zake za utatuzi wa migogoro kwa nchi za Afrika hususani mgogoro uliozuka Kenya baada ya uchaguzi. Rais Kikwete yupo nchini Uturuki kwa ziara rasmi ya kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Uturuki, na anatarajiwa kuondoka Jumapili kuelekea Jordan kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Mfalme Abdullah II.

Haya mdau...safari moja huanzisha nyingine...na nyingine..., Rais wetu anazidi kuzikwaa nondozz za Uzamivu za heshima



1 comment:

  1. Kuna wakati najiuliza sana Heshima za PHD za namna hii hasa baada ya kucheki waliokua wanampa Robert Mgabe PHD za namna hii walipoanza kutamka wamfikiriavyo kikweli hadharani.

    ReplyDelete