28/03/2010

"Sama" imeanza huku!


Kunradhi wadau kwa kutoweka kwa kipindi cha siku kadhaa kutokana na kubanwa vilivyo na majukumu!Leo huku kwa wenzetu Ulaya, Summer ndo imeanza. Naona angalau kidogo labda "kajua jua" katachukua hatamu ingawa "samtaimz" hali haitabiriki. Lisaa limoja limesogezwa mbele kwa kile wanachokiita "daylight saving time" inayoanza leo mpaka Jumapili ya mwisho ya mwezi Oktoba. Haya na tusubiri hako "kajua"!

4 comments:

 1. Hali kazi kwelikweli nilikuwa night leo kwa hiyo nimefanya kazi ya kusogeza hilo lisaa limoja kila saa ilioyopo ukutani. Haya na sasa ile michomo na watu wote waliojifungia ndani sasa utaona wanatoka nje wamepauka kabisa kwa kukosa jua. Upendo Daima!!

  ReplyDelete
 2. Pole sana dada Yasinta kwa libeneke la saa. Mbona kazi kwelikweli!

  ReplyDelete
 3. Ahsante kaka Mathew. Ndo maisha na pia ni moja ya kazi!!

  ReplyDelete
 4. Kabisa dada yangu!Bila pilika mambo hayaendi.

  ReplyDelete