Rafiki yangu leo amekumbuka miaka mitano tangu kufariki kwa mama yake. Nimeona vyema kuisindikiza siku hii muhimu kwa tungo hizi chache...
Nakukumbuka mama yangu
Mpendwa nafsini mwangu
Napovuta pumzi zangu
Wabaki kichwani kwangu
Mama, pendo lako ni hazina!
Wema wako kwetu mama
Kamwe hatutoupima
Leo nadiriki kusema
Ulituacha mapema
Mama, ungekaa nasi zaidi!
Mama yetu ulitutunza
Maadili ukatufunza
Wala hukutufukuza
Siku zote ulitujuza
Mama, kamwe hukuchoka!
Ulihimiza tupendane
Na pia tusaidiane
Hukutaka tutengane
Hukupenda tushindane
Mama, twayakumbuka haya!
Sasa miaka mitano
Unabaki wa mfano
Twajua kuna makutano
Na kushikana mikono
Mama,daima tutakuenzi!
Pole sana kwa kufiwa na mama kwani hakuna kitu kinachoweza kufananishwa na mama. Amekutoka lakini yupo nawe na tuzizi kuwombea. Amina
ReplyDelete