10/03/2010

Madereva Teksi Wanapogoma!

Kizaazaa cha masaa kadhaa kiliibuka baada ya madereva wa teksi kugoma katikati ya mji wa Dublin, na kwenye viwanja vya ndege vya Dublin, Cork na Shannon. Kugoma huko kunafuatia kile wanachodai kupinga sheria mpya inayowataka kufanya mtihani wa majaribio ya uelewa wa sheria za utoaji huduma hiyo, ufahamu wa vyombo vyao vya usafiri na jinsi wanavyoweza kukabiliana na dharula. Sanjari na kupinga, madereva hao wanagoma kushinikiza wenzao wawili wanaoendelea kugoma kwa amani kwa takribani masaa 19 yaliyopita katika ofisi ya Mdhibiti Teksi Dublin, waruhusiwe kutumia vyoo na kupata chakula katika ofisi hiyo.

Katikati ya mji wa Dublin, madereva hao walipaki magari yao na kuyaacha barabarani na kuendelea kuchapa stori katika mitaa ya O' Connell na Fitzwilliam Square na kusababisha msongamano mkubwa wa magari. Ilikuwa ni kaazii kweli kweli!Polisi walilazimika kufanya kazi ya ziada kuongoza magari

Hapa madereva wamepaki na kuyaacha magari yao barabarani


Foleni barabarani

Hapa madereva wanachapa storiNo comments:

Post a Comment