15/04/2010

Msaada Tutani toka kwa Makulilo, Jr.

Kutokana na wingi wa uhabarishaji wa masuala la udhamini wa elimu ya juu ughaibuni (Scholarships overseas), nimeanzisha SCHOLARSHIP PROFILE ambayo mtu akijiunga itasaidia kupata scholarship information kila wakati, na kujibiwa maswali yako mara nyingi. Unaweza kujinga hapa http://www.facebook.com/makulilo.scholarships

Hii itasaidia kwa upande wangu kuwafikishia ujumbe watu wengi sana, na kwa urahisi. Pia itanisaidia kuwa na idadi ya watu wachache, marafiki tu kwenye facebook page yangu ya masuala binafsi.

Pia ubnaweza kujiunga na SCHOLARSHIP FORUM www.scholarshipnetwork.ning.com na kuweza kuwa unapata scholarship update kila mpya inapowekwa mtandaoni hapo. Hiyo itakusaidia sio kila wakati kutaka kukariri na kukumbuka tovuti yangu, na pia itakuwezesha kupata e-mail kwenye inbox yako na kuweza ku-forward kwa watu wengine unaowafahamu nao waweze kuzifanyia kazi taarifa hizi za scholarship.

Kumbuka tu MAKULILO BLOG www.makulilo.blogspot.com bado ipo pale pale, itaendelea kuwakilisha daima.

Nawashukuru wadau wote mnaotembelea links ninazoweka mtandaoni na kuzifanyia kazi.

MAKULILO, Jr.

San Diego, CA

No comments:

Post a Comment