19/02/2011

Salamu ya Asubuhi


Umeamkaje mwandani,
Mpenzi wangu wa moyoni,
Nakusalimu gudimoni,
Uliyenikaa akilini.

Patina wa maisha yangu
Niliyezawadiwa na Mungu
Unayegusa mtima wangu
Hubanduki mawazoni mwangu.

Ninakupenda mpenzi,
Penzi langu silegezi,
Atujalie Mwenyezi,
Tuifikie ile enzi.

Nitakuja hadi ukweni,
Kule kwetu nyumbani,
Watufukize na ubani,
Tupate baraka maishani.

Nakushukuru mwandani,
Mwenzi wangu maishani,
Nakuahidi asilani,
Hutobanduka moyoni.

Endelea kunipenda,
Kamwe sintokutenda,
Nitakutunza kama kinda,
Na popote sitokwenda.

5 comments:

 1. bonge la salamu,
  wala haiishi hamu,
  moyoni li tamu.

  ReplyDelete
 2. Nakubaliana na Mt na pia mtani fadhy ni bonge la salamu yaani mtu unaamka asubuhi na kuzipata salamu kama hizo mmmhhh! basi naacha kuwaza kwa sauti...

  ReplyDelete
 3. ..au unaamka asubuhi na kutoa salamu kama hizo mmmmh!!

  ReplyDelete