11/03/2011

Hutofutika Moyoni!


Hutofutika moyoni
Hutonitoka rohoni
Utabakia maishani
Taabuni na furahani

Umeiweka alama
Itabaki imesimama
Moyoni imezama
Haiwezi kunihama

Mimi nilipofikia
Siwezi kujisifia
Ni wewe nakusifia
Na Muumba yarabia

Sikuoni machoni
Sikusikii masikioni
Nakuona taswirani
Nakuwaza akilini

Wewe ni tunu yangu
Ewe mzazi wangu
Nitakukumbuka mama yangu
Siku za maisha yangu!


Kwa rafiki yangu mpendwa anayekumbuka miaka sita leo toka mama mpendwa atangulie mbele ya haki.

2 comments:

 1. Tupo pamoja kaka.
  Ni kweli hakuna kama mama
  Tumwombee kwa sala.Amina

  ReplyDelete
 2. Pole Mkuu!

  Nimatumaini yangu katika kumbukumbu huumii tu lakini,...


  .... kwa kuwa naamini MAMA angependa uendeleze libeneke kwa furaha kwa baraka zake pia!

  Ni wazo langu tu kwa sauti Mkuu!

  ReplyDelete