01/04/2011

Mwanasosholojia Apata Ajali: Agongwa na Basi!

Leo Mwanasosholojia amepata ajali na kuvunjika mguu wa kulia na kiuno baada ya kugongwa na basi (pichani chini). Hivi sasa amelazwa katika hospitali ya St. Vincent kwa matibabu na bado anajisikia maumivu makali. Ripoti ya awali ya madaktari inaonesha kuwa amevunjika mfupa mkubwa katika mguu wake wa kulia na pia mfupa wa nyonga. Ajali ilitokea wakati akivuka barabara katikati ya jiji la Dublin, mtaa wa Marlborough, akijaribu kuwahi taa zilizokuwa zimeruhusu magari akitegemea kuwa angeweza kuvuka kabla ya basi lililokuwa likija kwa kasi kumfikia. Bahati aliwahi kukimbizwa hospitali na wasamaria wema akiwa amepoteza fahamu.
Basi lililomgonga Mwanasosholojia

14 comments:

 1. Pole sana....unaendeleaje lkn kwa sasa?get well soon mwanasologia

  ReplyDelete
 2. Pole sana mkuu..Tunakuombea upone haraka na kwendelea na shughuli zako..

  Tuko pamoja!

  ReplyDelete
 3. Pole sana kaka na nakuombea upone haraka Mungu yu nawe...

  ReplyDelete
 4. Umewapata, siku ya wajinga duniani!

  ReplyDelete
 5. Pole sana, Mungu mponye kaka yetu kwa Jina la Yesu Amen.

  ReplyDelete
 6. Pole sana Kaka. Mungu akuponye haraka

  ReplyDelete
 7. Bado najiuliza hapa Mkuu kuhusu kama haujatudaka maana hii April 1 /siku ya wajinga inamambo yake!
  Si unajua tena kama umegongwa hivyo na uko kwenye komputa DUH!

  Nawaza tu!

  ReplyDelete
 8. kama kweli ni haya mambo ya wajinga ka hapu juu asiye na jina alivyosema "Anonymous said...
  Umewapata, siku ya wajinga duniani!
  01/04/2011 14:10" Hakika utakuwa umefanya jambo ambalo si la utu kabisa. Maana naona hata Mt. naye anaanza kuweka wasiwasi. Tupe ukweli kaka Mathew ....

  ReplyDelete
 9. Si ndio hapo Mt Kitururu, mie mh!!!! :-))
  Mie nimeshaishtukia, maana nimehama nayo kutoka kwa Yasinta maana nilitaka kusema hii siku ya mazezeta

  ReplyDelete
 10. AAAAhhhhh Nguli, umewapata wa kutosha

  haya bwana.

  ReplyDelete
 11. hhahahhaha hii ilikua kiboko!! wengi husema wamegongwa na gari ivi ukisema hvyo watu wanaleta attention ama? duh kazi ipo mwaka huu!!!!!!!!

  ReplyDelete
 12. Lakini kwa kweli si jambo zuri kuwadanganya wapendwa wake kwa jambo kama hili ambao wanakupenda je siku itayotokea kwa ukweli unafikiri itakuwaje? binafsi niliumia sana tena mno na baada ya kupata habari kuwa ni sikukuu ya wajinga nilihuzunika sana kwa hili. Na bado najiuliza kwanini kutudanganya jambo kama hili???

  ReplyDelete
 13. Dada yangu Yasinta na rafiki zangu wengine wote wapendwa, narudia tena kuwataka radhi sana kwa usumbufu ambao umejitokeza katika siku hii ambayo kwa mtizamo niliokuwa nao, huwa haichagui aina ya utani.Nisingeweza kufanya hivyo asilani katika siku nyingine yoyote. Ni kweli, nilikosea kwa kuingiza utani katika suala ambalo katika hali ya kawaida ni sensitive. Narudia tena kusema samahani sana lakini nimezidi kutambua umuhimu wa marafiki na kublogu katika kushirikishana na kuitikia mambo mbali mbali, yawe ya utani au ya ukweli.

  ReplyDelete