01/04/2011

Mwanasosholojia yu Buheri wa Afya

Jamani wadau na wanalibeneke, Mwanasosholojia yu buheri wa afya anaendeleza libeneke kama kawaida na wala hajapata ajali. Kilichotokea ni kuisindikiza tu siku hii maarufu ya Aprili moja kwa haka ka "prank". Anawashukuru sana wale wote waliompa pole baada ya kupata habari za utani huu. Anamshukuru pia da' Yasinta wa blog ya Maisha na Mafanikio  na Mwanazuoni Chambi Chachage wa Udadisi kwa kuusambaza utani huu kupitia blog na barua pepe. Kikubwa, anachukua nafasi hii kuwataka radhi sana kwa usumbufu ambao umejitokeza  lakini amezidi kutambua umuhimu wa marafiki na kublogu katika kushirikishana na kuitikia mambo mbali mbali, yawe ya utani au ya ukweli.  

1 comment: