23/04/2011

Tuzo kwa Mabloga!

We are pleased to announce our 1st annual online Tanzanian Blog Awards! These awards will honor the courage, impressive, educational, creative Tanzanian bloggers all over the world.
 
How to Nominate:
To enter the Tanzanian Blog Awards you can fill a nomination form that is available on our blog www.tanzanianblogawards.com if you not able to access that form just send an email to tanzanianblogawards@gmail.com with the following information:

Name of Nominee (used by blogger publisher)

Current Location (City/Province/State/Country)
Blogsite Name (That appears on Header)
Blog URL Link (html address)
Blog Category (Personal Diary, Family, Humor, Political, Religious, etc)
Last day to nominate your favorite is May, 31st 2011…If you can access our online nomination form then send your nominations to tanzanianblogawards@gmail.com
Follow us on twitter: Bongobloggers for more update. 


Haya wadau...kazi kwenu kupendekeza! 

6 comments:

 1. Mtakatifu kulikoni wawaza kwa kuguna tena?

  ReplyDelete
 2. @Mwasosholojia: Mguno ni bomba la kusema ulichosema nimekipata katika mguno huo hapo juuu!

  ReplyDelete
 3. @Mtakatifu nimekusoma mkuu..teh!teh!Tunakwenda kibongobongo kama kawaida.

  ReplyDelete
 4. Mwenyekiti Wa Kibaraza, kwa heshima yako!


  Nakutembelea leo mara ya kwanza.


  Juu yako, naufurahia na kuusherehekea uAfrika wangu kwa kuona inaelekea nchi Tanzania huthamini wanablogu. Kama nakosea naomba usahihisho.


  Nchi zingine kama huku kwetu (kutokana na mfumo wa kale wa ubaguzi wa rangi uliowanyima Waswahili huku elimu ya kutosha) bado tunaviongozi (tena Waswahili-wenzetu wanaodai wao ni "wanamapinduzi" na "wapigania-uhuru") wanaolala na kula hisia za kijinga kwamba eti "wanablogu na waandishi wa habari pia ni adui za jadi kwa serikali yao".

  Kama ninavyokwandikia hivi leo, blogu yangu kwa lugha ya Kiingereza ambamo nilikuwa namwandikia Raisi wetu barua wazi kuhusu ukabila na XENOPHOBIA nchini humu imefungwa na serikali tarehe 05 April 2011.


  Madai dhidhi yangu: eti 'Manyanya wewe unawatukana wakubwa wa serikali na tunakufungulia mashtaka kwanzia leo' wakati ukweli ni kwamba nilikuwa nataja majina ya mafisadi na "viongozi" wenye ukabila serikalini iliyeanzishwa na libabu limoja (sipendi kutaja jina) mnamo 1994.

  Kazi kweli leo kuwa Mwafrika-Kusini mwenye mawazo yake!!! Hakika leo Afrika Kusini huwezi ukatoa mashindano ya wanablogu wanaochukiwa vile kama paka mlavifaranga!


  Kwa hiyo, natoa kofia tena kwa taifa la Tanzania na serikali yenu kwa mwamko wenu kuhusu umuhimu wa hoja kutokana na BLOGGING.

  Hapo ningependa kuishia, lakini...

  Kwa yote, wacha nimalizie kwa kumshukuru Muumba kwakuwa niliwahi kukanyaga nchini Tanzania (1985-1994) ili nami niwe najizatiti katika lugha (Kiswahili) kubwa kuliko zote Barani Afrika, kienyeji yaani.


  Mimi lugha yangu niSiswati/Kiswati inaongelewa Ufalme wa Swaziland na Jamhuri ya Afrika Kusini (jimbo la Mpumalanga).


  Labda utaniuliza: "ulikuwa Tanzania kivipi?"


  Nilikuwa mkimbizi au Mpigania-uhuru enzi hizo. Nilikuwa kwanza Morogoro sehemu za Dakawa. Baadaye, Mlandizi sehemu za Masuguri. Baada ya hapo: Dar es-Salaam sehemu za Ubungo Kisiwani ambamo hadi leo hii ninandugu zangu wa damu, Watanzania.


  Baadaye nilikaa Dar es-Salaam jijini karibu na kituo cha Mnazimmoja kwenye jengo "Mwananchi", Mtaa (nahisi) "Samora Machel".


  Enzi hizo niliwahi, kwa jina-bandia la "Alphonse Mpili" kuwa hata moja wa walimu wa hesabu huko Upanga, Shule Shaaban Robert c.1988.


  Kwa jina-bandia (tena) la "Mordecai King", (c.1991-1994 hukohuko jijini Dar es-Salaam pia nilikuwa mtangazaji Radio Tanzania Dar es-Salaam wa vipindi kwa niaba ya moja ya vyama vya ukombozi: Pan Africanist Congress of Azania/South Africa.

  Mimi pia ni "mwenyeji" sana Iringa (Kijiji cha Mninga) pale nilipopatia mama (Leonilde Makafu) wa kwanza kwa watoto wangu Thoko ("Furaha" ya Kizulu) Maziri (kutokana na jina "Maziriankhunda Phiri" ambalo ni jina lake baba yake babu yangu), pia na Tamara ("Mtoto wamwisho" kwa Kitumbuka ambacho ni lugha ya kabila langu katika taifa la Wanyasa huko Malawi kaskazini sehemu za Mji Chilumba.)

  Mwisho kabisa: nawaombea sana Watanzania wasiache uongozi wao katika bara letu kuhusu mfano wa kuigwa katika suala: "UTU NDIO NINI? NAO UBINADAMU NI KITU GANI?"

  ReplyDelete
 5. Karibu sana Phiri!

  Lazima nikiri, sikuyajua haya na nimeguswa sana na maelezo yako pamoja na historia yako. Nisifiche, nimeshikwa na bumbuwazi na nachukua fursa hii kutafakari zaidi ili kuweza kutamka chenye mantiki..otherwise kwa sasa, nimefurahi kupata mgeni kibarazani...karibu sana

  ReplyDelete