27/04/2011

Masanja Mkandamizaji kuwa Mchungaji?

 Masanja akihubiri na kuimba (Video kwa hisani ya GPL)

Msanii wa uchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi Emmanuel Mgaya almaarufu "Masanja Mkandamizaji" ameonekana akihubiri injili katika maeneo ya Karume, Ilala, Dar es Salaam. Masanja ambaye ni muumini wa kanisa la EAGT, Mito ya Baraka lililopo Jangwani, Dar es Salaam alisikika akikiri kupenda kuwa mchungaji na kuwaomba watu waliokuwa wakimsikiliza kuokoka ili kuwa kama yeye.

Huu ni moja ya usanii  wa Masanja au amenena kwa dhamira ya dhati? Yetu macho na masikio

2 comments:

  1. Duninani chochote chawezekana!

    ReplyDelete
  2. Asituchang'anye akili huyo!

    Napendekeza atumiwe huyo barua haraka iwezekanavyo ili abebe mfukoni mwake kofia mbili na kwa kila alitendalo achague atavaaa kofia yenye maandishi gani: "kofia ya Masanja" au "kofia ya dhamira ya dhati"?

    ReplyDelete