03/05/2011

Osama Aliponzwa na Mesenja wake!

Makazi alimokutwa na kuuawa Osama bin Laden
Ni karibu mwaka sasa tangu siku mmoja wa wasaidizi wa karibu wa marehemu Osama bin Laden alipopokea simu yake ya mkononi, simu ambayo bila yeye mwenywe kujua, ilitumika kulipeleka jeshi la Marekani hadi mlangoni kwa bosi wake.

Mmoja wa maofisa wa Kimarekani aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatatu kwamba simu ile alipigiwa mmoja wa mesenja (tarishi) wa Osama ambaye alikuwa akifuatiliwa na majasusi wa Kimarekani kwa karibu mwaka mzima. Mesenja huyu ndiye aliyefanikisha kufichua maficho ya Osama aliyekuwa akiishi katika eneo la watu matajiri na wanajeshi wastaafu huko kaskazini mashariki ya Pakistani.

Osama alikuwa akiishi umbali wa kilomita moja toka chuo cha kijeshi cha Pakistani, na wala sio mapangoni kama ilivyokuwa ikifikiriwa miaka nenda rudi. Osama alijikuta akivamiwa na makomandoo wa Kimarekani alfajiri ya Jumatatu, kwa saa za Afrika Mashariki, na kusambaratishwa ndani ya dakika 45, baada ya kuwaponyoka Wamarekani kwa takribani miaka 10 tangu shambulizi la Septemba 11, 2001. Majasusi wa Kimarekani wanasema Osama alikuwa akiishi kwenye nyumba yenye jumba la kifahari, uzio mrefu na wenye nyaya za umeme kwa juu, na pia ilikuwa ni nyumba yenye uwanja mkubwa.

Majasusi wa Kimarekani wamekuwa siku zote wakisema kwamba hapakuwa na njia nyingine ya kumkamata Osama bali walichokuwa wakiweza kufanya ni kusibiri afanye makosa yeye mwenywe. Siku zote walikuwa wakiamini kwamba njia rahisi kabisa ya kufikia Osama ilikuwa ni kupitia wasaidizi wake, kama huyo mesenja wake. Majasusi hawa waliamini kwamba mesenja huyu ndiye mtu pekee ambaye huenda Osama alikuwa akimwamini kabisa kwamba asingeweza kumsaliti.

Majasusi hawa wa Kimarekani ambao wamekuwa wakifatilia mchezo huu kwa kitambo walisema Osama alikuwa ni mtu wa kuwasiliana na watu wake kwa rekodi za audio au video, lakini ili kufikisha jumbe zake alihitaji mtu wa kuchukua jumbe hizo na kuziwasilisha sehemu husika, ndipo mesenja huyu alipoingizwa kwenye gemu.
 
Soma zaidi gonga hapa Fotobaraza

2 comments: