10/07/2011

Hongera Sudani ya Kusini!

Tarehe 9 Mwezi Julai, 2011 Sudani ya Kusini imekuwa taifa jipya duniani baada ya kujitenga rasmi na kujitangazia uhuru wake. 
Baada ya vita vya muda mrefu vya umwagaji damu, Sudani ya Kusini sasa inajitawala huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali za ndani na za nje ya nchi. 
Kwa umoja, mshikamano na kujituma Kibaraza hiki kinategemea kuwa taifa hili litayashinda na kuyakabili yote na kuwa moja ya mataifa thabiti hapa Afrika na duniani. 
Hongera sana Sudani ya Kusini.

No comments:

Post a Comment