28/07/2011

Kumpata Mke Balaa...


Bwana mmoja nchini Marekani hatimaye amefunga ndoa kwa mara ya kwanza, baada ya kusaka mchumba kwa zaidi ya miaka sabini.


Bwana huyo Gilbert Harrick mwenye umri wa miaka tisini na tisa sasa ambaye alipigana katika vita vya pili vya dunia amesema hakuwahi kukutana na msichana aliyempenda kwa miaka yote hiyo.


Bwana Gilbert amefunga ndoa na Bi Virginia Hartman mwenye umri wa miaka themanini na sita.


Gazeti la Rochester Cronicle limesema wawili hao kwa sasa wanaishi katika nyumba ya kutunza wazee, mjini New York.


"Tulitaka tuishi pamoja katika chumba kimoja, lakini walitukatalia hadi tufunge ndoa" amesema bwana Gilbert, "Kwa hiyo nikamuomba tuoane na yeye akakubali" ameongeza mzee huyo.

Kabla ya kuoana na kuishi katika chumba kimoja, wapenzi hao walikuwa wakiandikiana barua za mapenzi kila mara.


"Ni wazimu, lakini ndio raha yenyewe" amesema Bi Virginia, ambaye ana watoto watano katika ndoa yake ya awali.

CHANZO BOFYA HAPA

4 comments:

 1. Hivi mtu anapopost comment "No comment!!!" ina maana gani?

  ReplyDelete
 2. Huyu jamaa alikuwa anataka tu roommate na wala sio Mke! SI inamaana wangeruhusiwa kukaa chumba kimoja asingefikiria kuoa?

  ReplyDelete
 3. Ha haaa.. babu mjanja huyu. Angeruhusiwa kukaa naye chumba kimoja asingefunga naye ndoa. Ha haaa

  Mama Malaika

  ReplyDelete