21/07/2011

Utani Mwingine Bwana....!

Iringa mjini
 Nimeikuta hii sehemu, nikaona "niimuvuzishe" hapa kibarazani...
TANGAZO KWA WAHEHE WOTE:
Chuo kipya kabisa cha Kihehe kimefunguliwa Kihesa, Iringa.
(HEHE SKILLS AND TECHINICAL COLLEGE OF LIFE)
Kinatangaza kozi za mwaka 2011/2012 kama ifuatavyo,
1.Kugema ulanzi miezi 6
2.Kusokota kamba za kujinyonga miezi 9
3.Kuchagua mbwa anaefaa kuliwa na mapishi yake miezi 8
4.Kuongeza hasira miezi 10-12
Atakae jiunga mapema atapewa kozi ya upishi wa Mkunungu pamoja na uoshaji wa Mbeta.
Utani mwingine nao....si mchezo!

4 comments:

 1. Nimecheka hadi basi.Mtunzi wa utani huu kawapatia Vanyalukolo huko Tanangozi,Rungemba,Kalenga,Kidamali,Ilula n.k. Hongera!

  ReplyDelete
 2. Hahahhaha Ahsante sana kaka Ujumbe umefika!

  ReplyDelete
 3. Nimecheka mpaka machozi yametoka hahhahahhaha!!! well nimetoa single pia huko kibarazani kwangu karibuni lol

  ReplyDelete
 4. Mimi ni Mwagito kutoka Iringa.Nimerudia kuusoma utani huu sijui mara ngapi. Kila ninaposoma nacheka saaana.Si kutokana na utani wenyewe tu ambao tuliusikia tangia tungali wadogo.Tukakua tukijua ni utani tu hadi hii leo na utabakia ni utani.Kilichonifurahisha ni UBUNIFU wa huyu aliyeviweka vipengele hivi pamoja na hivi habari hii kuonekana kama ya kweli jinsi tangazo linavyoanza maana siku hizi matangazo ya shule, vyuo ni mengi.Umeniacha hoi kabisa.Sasa narudia tena kusoma.Kila nitakapokuwa nataka kufurahi na kuondoa msongo wa mawazo nitakuwa nasoma tangazo hili.Ni mimi Mwagito va kunyumba.

  ReplyDelete