08/08/2011

Babu wa Loliondo aiponza Serikali

Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapila a.k.a "Babu wa Loliondo"
 
Hapo nyuma nilitoa ushuuda wangu kuhusiana na kikombe cha babu. Baada ya kupata kikombe changu, nilirudi zangu DAR. Siku 12 zikapita nikawa situmii ARV's matokeo hali yangu ikawa mbaya sana ikabidi nikimbizwe hospitalini. Ilinibidi kuzirudia ARV na sasa hali yangu imeimarika kiasi. Rafiki yangu, mwenye virusi vya ukimwi naye alienda kwa babu, aliporudi alianza  kutangaza kwamba kapona. matokeo yake hali yake ikawa mbaya ghafla na kufariki dunia.

Nadiriki kusema wazi kwamba  sidhani yupo hata mmoja aliyepona kwa babu. Kule loliondo nilikutana na watu wengi zaidi ya 10 ambao walifariki wakiwa kwenye foleni, na wengi wao kutokana na ugumu wa maisha walisogea umbali mfupi na kuzitupa miili ya ndugu zao. Nashangaa hadi leo serikali haijatoa tamko kuhusu watu wanaopoteza maisha yao loliondo, wala haijatoa tamko rasmi kuhusu tiba ya babu. Mbaya zaidi, Synnovate wamedandia hili sakata kwa kudanganya umma kwamba 78% ya waliokunywa dawa wamepona

Kabla sijaenda loliondo, ndugu zangu  pamoja na marafiki walikatiza sana moyo kwenda, ila kutokana na hali yangu ya kuichungulia mauti, sikuwa na jinsi. Nililazimika kwenda kutafuta tiba ya loliondo. Cha kushangaza zaidi, baadhi ya hawa ndugu na marafiki nao ni waathirika wa virusi vya ukimwi ambao wanatafuta tiba.Wiki chache baadaye, magazeti na vyombo vingine vya habari vilipambwa na viongozi wa kitaifa waliokwenda kwa babu wakionyesha umma kwamba dawa ya babu kweli ilikuwa tiba kwa mafano "Augustino Mrema"  alisema kapona kisukari.
 
Matokeo yake hata wale waliokuwa wakinikejeli waliondoka na kwenda kwa babu. Hadi naandika hii barua, wawili kati yao wamefariki baada ya kurudi wakiamini wamepona. mwingine kapandwa na ukichaa baada ya hali yake kuzorota zaidi, na mda wowote anaweza kututoka.Bila viongozi wa serikali kwenda loliondo ndugu zangu na mafariki wasingekufa haraka hivi.

Nadiriki kusema kwamba, naifungulia serikali yetu mashtaka kutokana na vifo vya ndugu zangu wawili na marafiki watatu kutokana na kuudanganya umma. Nazifungulia vyombo vya habari vilivyoshirika kuiadaa umma, pamoja na kampuni ya Synnovate ambayo imezidi kuikoroga jamii wakidai kwamba 78% ya waliokunya kikombe cha babu wamepona. Kwanza serikali ilitudanganya ikisema kwamba ingepima  dawa hiyo ya babu na kutujulisha kama kweli inatibu magonjwa sugu anayodai babu. 

Hadi leo serikali imekaa kimya. Viongozi wengi wa kitaifa wamekimbilia loliondo, kitu ambacho kiliwafanya ndugu zangu ambao hali yao ilikuwa nzuri kuamini kwamba, kama viongozi wanakimbilia loliondo basi nao waende ili wapone, matokeo yake wakafa. Kwa maana hiyo naifungulia serikali makosa mengi ya jinai na udanganyifu. Navishtaki vyombo vya habari pamoja na serikali  kwa kutokuwajali wananchi wake. Nakumbuka Maggid mjengwa, John mashaka, pamoja na kaka mmoja anayeitwa mwilima walileta mijadala  mikali sana kuhusiana na loliondo tukidhania serikali ingechukua jukumu la kuiambia umma ukweli kuhusiana na loliondo ambalo limegeuka kuwa machinjo ya watanzania wasio na hatia.
 
Mdau Mallya
 
CHANZO: "Kliki" HAPA 
 
Imekaa kaa vipi hii wadau?

2 comments:

  1. "Viongozi wengi wa kitaifa wamekimbilia loliondo, kitu ambacho kiliwafanya ndugu zangu ...kuamini kwamba, kama viongozi wanakimbilia loliondo basi nao waende ili wapone"

    WACHA MANTIKI HIYO WEEE! KUNYWA VIDONGE!!! (SASA UKIMUONA RAISI WA NCHI YAKO KWA MFANO LABDA ANAIBA PESA NA HAJAKAMATWA NAWE UTAKWENDA IBA?)

    ReplyDelete
  2. ANGELA JULIUS03/10/2011, 15:30

    BINAFSI HII TIBA TANGU MWANZO MOYONI MWANGU HAIKWEPO KABISA WALA SIKUWA NAISHABIKIA KUNA MTU ALINIOMBA NIMKOPESHE PESA KIDGO YA KWENDA LOLIONDO NIKAMJIBU SITAKI KUSABABISHA KIFO CHAKO NI BORA UNGENIAMBIA KWA SABABU NYINGINE LABDA NINGEKUFIKILIA HAKUONGEA NA MIMI BAADA YA HAPO MUDA MFUPI KURUDI LOLIONDO TUKAELEWANA ILA KWA KWELI HAKUFIKA MBALI ALIPOTEZA UHAI WAKE, MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI AMEIN

    ReplyDelete