16/08/2011

Mjamzito aliyenyanyaswa Kulipwa Fidia


Aliyekuwa mhudumu wa mgahawa aliyefukuzwa kazi akiwa mjamzito, atalipwa fidia ya zaidi ya Euro 14,000.

Dada huyo ajulikanaye kama  Jevgenija Petrakova, alikuwa aifanya kazi katika mgahawa uitwao The Admiral, uliopo mtaa wa Marlborough, mjini Dublin, Ireland. Alifanya kazi kwa wiki sita tu kabla ya kuachishwa tarehe 30 mwezi Machi, 2009.

Awali ilidaiwa mahakamani kuwa Jevgenija alitengwa, kuteswa na kunyanyaswa kijinsia kabla ya kuachishwa kazi kwa kigezo cha jinsia, utaifa na ujauzito wake.

Kampuni ya  Lexor Entertainment Limited, ambayo inamiliki mgahawa huo unaotoa huduma ya vyakula vyenye asili ya Russia iliyakataa malalamiko ya Jevgenija.

Mahakama ilibainisha kuwa mlalamikaji (Jevgenija) hakuweza kuithibitishia juu ya malalamiko ya unyanyasaji aliodai kufanyiwa, lakini iliridhishwa na malalamiko ya kufukuzwa kwa kigezo cha jinsia na kuuamuru mgahawa wa The Admiral kumlipa mlalamikaji fidia ya Euro 14,167.92 ambayo ni sawa na mshahara wa miezi tisa.

Zaidi soma HAPA

Imekaaje hii kama ingekuwa kwetu Bongo? Wangapi wananyanyaswa na waajiri na kushindwa hata kufungua kesi? Na wanaoweza kufungua wanashinda kesi hizo au waajiri ndio wanaoibuka washindi? Maswali lukuki....

1 comment: