26/08/2011

Vipaji vingine...mmmmh!

Hapan'shaka huyu binti ana kipaji cha kipekee cha kukariri...

Video kwa hisani ya mdau mkubwa wa kibaraza hiki, Dezidery Kajuna

12 comments:

  1. WOOOWWWWWWW! hakika huyu binti ana kipaji kama kweli ni kipaji..

    ReplyDelete
  2. Mimi nafikiri ana kipaji cha kukariri, na kuna uwezekano amekaririshwa hiyo miji mikuu ya nchi zote hizo na haimbanduki kichwani

    ReplyDelete
  3. hata hivyo kaka M. mtoto kama huyo kukariri hivyo kweli?..au labda kuna mtu alisimama na kibao naye alikuwa anasoma mmmhh ila haiwezekani ajue kusoma ? Sijui sasa...

    ReplyDelete
  4. Unaweza kujiuliza maswali lukuki Da'Yasinta,maana huyu binti hakuwa anaonekana anasoma chochote, ndio maana kuna kipindi alionekana kama amesahau mji fulani kidogo na baadaye anaukumbuka. Nafikiri ni kipaji tu ingawa sijui amekaririshwa vipi...:-)

    ReplyDelete
  5. Duuh, kama sio ujanja wa komputa basi hiki ni kichwa.....!

    ReplyDelete
  6. Mtoto KICHWA huyu! Ila wapo watoto kibao wa hivi aisee! Wanakuambia ukiingia kwa mfano mitaa kama Pakistani au sehemu ambayo MADRASSA ni shule. Unaweza kukuta karibu katika kila madrassa kuna katoto ambako kadogo na kamesha kariri KURUANI hata ukaambie kaanzie wapi kanaanzia hapo bila makosa. na kwa mtoto mdogo KURANI ni kitabu kikubwa sana kukikariri bila kosa kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

    Fikiria tu wewe na ukubwa wako uambiwe ukariri BIBLIA neno kwa neno kuanzia mwanzo mpaka mwisho na hata ukurupushwe kutoka usingizini uulizwe mstari wowote wa BIBLIA na uukumbuke bila kukosea ! Sasa unakuta mtoto anamiaka mitano kwenye KURANI anafanya hivyo si maajabu hayo? Sikuhizi huwa wanampaka mashindano yafanyikayo MISRI kila mwaka ya vipaji vya kukariri KURANI na huwa nazinguka sana hasa na watoto wadogo kabisa na vipaji vyao hivyo.

    Ndio kuna wenye vipaji vya kukariri!

    Tatizo ni uelewaji saa nyingine lakini! KWa kuwa unaweza kujikuta umekariri kitu na kwa hilo unafaulu hata mitihani lakini hujaelewa kitu!

    ReplyDelete
  7. Yupo Mchungaji mmoja anaitwa Randy Skeet, ni mtu mzima amekariri Biblia YOTE!!

    Anakwambia fungua kitabu fulani ukishapa anaanza kusema bila kusahau nukta, koma, alama ya mshangao na kuuliza vyote haviachi.

    Hili la huyu mtoto linawezekana sana tu na hata wewe mzazi unaweza fanyisha mtoto wako mazoezi flani flani maalum kwa ajili ya uwezo wa kumbukumbu au vipo vyakula ambavyo ukianza kmpa mwanao kuanzia hivi sasa atakuwa na uwezo wa AJABU wa kumbukumbu.

    Watoto wa hivyo wapo wengi tu.

    Mimi wa kwangu nitahakikisha hanywi kinywaji chenye sukari atifisho kama soda n.k hadi hapo atakapofikisha umri flani hivi huku akiwa chini ya mafunzo maalum ambayo akiyapata akingali mdogo yakamkaa hautambadilisha kamwe.

    ReplyDelete
  8. Mkuu Mcharia, shukrani, umenifumbua macho hasa kuhusu hilo la vyakula na vinywaji..:-)

    ReplyDelete
  9. Duuh kumbe soda kwa watoto mbaya eee!
    kuanzia sasa hata mi soda pia watoto wangu soda ni sawa na kituo cha polisi.
    Pilly

    ReplyDelete
  10. @Rasta Mcharia: Kuhusu madhara ya vyakula atifisho ambavyo ni ghali - Si basi masikini wangekuwa na miakili na kumbukumbu lukuki sana kwa kuwa kwao yasemekana hata cocacola ni za sikukuu kitu kifanyacho watoto wao mpaka umri fulani ni fulu mchicha ?

    Nakuzingua tu Mkuu!:-)

    ReplyDelete