17/10/2009

Unapokutana na Mdau Ughaibuni


Mwanasosholojia amepata bahati ya kukutana na mdau rafiki yake wa siku nyingi Nyangusi Ndukai, wakati wa mkutano wa kimataifa wa Sustainable Global Development unaoendelea kufanyika chuo kikuu cha Limerick, Ireland. Nyangusi kwa sasa amehitimu shahada yake ya Uzamili katika fani ya Maendeleo ya Jamii katika chuo cha Kimmage Manor. Kwa pamoja wanahudhuria mkutano huo unaowakutanisha washiriki kutoka sehemu mbalimbali duniani wakijadiliana mambo yahusuyo maendeleo. Mwanasosholojia yeye aliwasilisha mada yake jana.

4 comments:

  1. Nakuona jinsi unavyojisikia kukutana na rafiki yako wa zamani katika maneno yako jinsi ulivyokuwa na furaha. Ni kweli ni raha sana kuwa na rafiki na pia kukutana nao. Rafiki ni bora kuliko mwana sesele.

    ReplyDelete
  2. Wewe dada Ngonyani...Castory Ngonyani ni Kaka yako? Nilipata kusoma na mtu anaitwa Castory huko Ilboru Secondary!! Kama ni kaka yako niambie aliko tafadhali.

    Kuhusu kukutana Ughaibuni...ukweli ni kwamba mie sikutarajia kukutana na mtu ananijua kwa jina achilia mbali kukutana na mdau wangu wa karibu hivi....hii ni kuprove kwamba milima tu ndiyo haikutani.

    Nyangusi

    ReplyDelete
  3. Hongereni sana vijana. Mambo haya yanapendeza kusikia. Nimefurahi kwamba mnahudhuria mikutano mikubwa namna hiyo! Nmnastahili pongezi za dhati.

    ReplyDelete
  4. Ndukay umeondoka lini nyumbani wewe? Haya tuwakilishe vyema huko!!!

    ReplyDelete