09/04/2009

Hizi ni Juhudi za Kweli za Kukwamua Wabongo katika Umasikini?

Vyanzo vya habari vinatueleza kuwa wananchi jijini Dar wameamua kuonesha waziwazi kutokubaliana na BoT kutaka kuifunga kampuni ya DECI (T) Limited. DECI kwa kirefu Development Entrepreneurship for Community Initiative inapigiwa upatu na wanachama wake wanaokadiriwa kufikia laki saba Bongo kuwa inawasaidia wenye kipato cha chini na cha kati kutokana na "Kuvuna Kadiri Ulivyo Panda". Lakini kumekuwepo na malalamiko mengi kuwa kampuni hii yenyewe ndo "Inavuna Kadiri Walala Hoi Wanavyopanda". Hapa kuna mgongano wa mawazo, na maswali yanayohitaji uwanda mpana kuyachambua kabla ya kuyatolea majibu.

Nimefurahishwa na Busara za Father Kidevu, Mroki Mroki. Waweza kugonga hapa http://mrokim.blogspot.com/2009/04/busara-za-mfuga-ndevu.html

Wewe una mawazo gani mdau wangu?


No comments:

Post a Comment