10/04/2009

Umeme kwa Walala Hoi Bongo

Huwa najiuliza maswali mara nyingi, hivi kuna siku moja walala hoi wote Bongo wataacha kutumia vibatari na kubonyeza "swichi" kuwasha umeme?Nia yangu si kuingia ndani katika dhana ya maendeleo, lakini najiuliza ukiondoa haya mambo ya mitambo ya Dowans na mengine pacha ya hayo, jitihada za kuwapatia nuru na maisha bora watanzania zinajikita sawa sawa vijijini? Nimekutana na hii habari nikaona ni vyema kuwashirikisha wadau;

Kikwazo cha Maendeleo Tarime Chaelezwa

WILAYA ya Tarime Mkoani Mara,hivi sasa imekumbwa na kukoekana kwa Umeme,na kukwamisha shughuli za biashara hasa zinazotumia Nishati hiyo,ikiwemo njia za mawasiliano na kupunguza kipato cha wananchi.

Kukosekana kwa nishati ya Umeme,kumewafanya wateja wa Shirika la Umeme TANESCO kwa kutovumbua tatizo hilo la miaka mingi,na kuwafanya mara nyingi kulala gizani,na kukwamisha huduma za kijamii,zikiwemo za maofisini.

Badhi ya watu waliozungumza na mwandishi wa habari hizi,wakiwemo wale wenye Komputa,Fotokopi,Faksi na vyombo mbalimbali vinavyotumia umeme,wamesema,wamekuwa wakipata hasara kubwa kwa kutofanya uzalishaji na kufikia hata hatua ya kufunga biashara zao kwa kukosekana kwa nishati hiyo.

Mwita Nyaikwabe ambaye ni mfanyabiashara Mjini hapa amesema kwamba,hivi sasa hauzi soda kutokana  kuwa za moto kwa kukosa Umeme ambao huzipooza na kuwa baridi huku Evance Onyango mwenye Internet CafĂ©,naye kudai kufunga shughuli zake kwa sababu za kukatika mara kwa mara kwa Umeme,Wilayani hapa.

Nao Waandishi wa habari walilalamika kukwamishwa kwa kazi yao ya kuuhabarisha, kuburudisha Umma kutokana na umeme huo ambao umegeuka kuwa kero na kuwalazimu kutumia habari kwa kukodi Jenerata kwa gharama kubwa na kukwamisa utendaji kazi wao.

Wateja hao wa TANESCO wameeleza kuwa,licha ya umeme kuwa kero kwa muda mrefu,wamekuwa wakipelekewa Ankara za malipo ya kiwango cha juu kuliko matumizi yao huku mara nyingi waatumia jenereta kwa kazi zao kuliko Umeme wa kusuasua.

Meneja wa Shirika hilo,Tawi la Tarime,Amos Mtai alipoulizwa kwa nini Umeme wa Tarime unakatika katika,na kuleta usumbufu na hasara kwa watumiaji,alisema tatizo ni Laini za nguzo kuanguka kutokana na kuoza kwa sababu ni za zamani sambamba na Tansfoma kulipuka kwa kuzidiwa  na nguvu ya Umeme huo.

Mtai alieleza kuwa uchakavu wa nguzo ni chanzo kinachosababisha kukatika kwa Umeme na kuahidi kuwa marekebisho yanaendelea kufanywa ili kuondoa usumbufu huo na kueleza pia kuwa siku zingine Shirika huzima Umeme na kuwatangazia wananchi kwa lengo la kupisha shughuli za kuunganiasha waya katika nguzo za chuma za umeme unaoenda katika Mgodi wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick Tanzania


Wadau, imekaa vizuri kweli hii??

No comments:

Post a Comment