10/04/2009

Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere yaja UDSM

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tunu ya taifa letu
Jumuiya ya wanazuoni katika chuo kikuu cha Dar es salaam, wanatarajia kuendesha wiki maalum la maadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius nyerere, kwa kushirikisha pia wanazuoni wengine toka nchi mbalimbali za kiafrika..

 Lengo la maadhimisho hayo, ni kuenzi falsafa za Mwalimu Nyere kuhusu elimu, na namna viongozi wa sasa wa kiafrika wanavyolipa umuhimu swala hili la elimu, ikilinganishwa na enzi za akina Nyerere na hayati Kwame Nkrumah.

 Mmoja wa wanazuoni wanaoratibu tamasha hili ni Prof Issa Shivji. Yeye anasema kamwe hatomsahau Mwl Nyerere kutokana na ukweli kwamba alikuwa chachu ya kunyanyua elimu sawa kwa watanzania wote

 Nao baadhi ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini wanasema kama kila kiongozi angekuwa muadilifu kama hayati mwl Nyerere hata masuala ya ufisadi ambayo yanaendelea kuitafuna Tanzania kila kukicha yangekuwa ni ndoto za mchana.

 Maadhimisho ya jumuiya ya wanazuoni na Mwalimu Nyerere yanataraji kufanyika kwenye chuo kikuu cha Dar es salaam kuanzia april 13 na kufikia kilele chake april 17, ya yatahudhuriwa na mwanazuoni maarufu barani afrika Profesa Wole Soyinka toka nchini Nigeria.


Undani kuhusu Mwalimu Nyerere waweza kuupata pia kwa kubofya hapa;http://www.infed.org/thinkers/et-nye.htm

No comments:

Post a Comment