24/05/2009

Kwaheri ya Muda Dublin, Ireland

Wadau, leo masaa machache yajayo, Mwanasosholojia anaiaga kwa muda Dublin. Anakwenda nyumbani Bongo kwa likizo. Kama mwanadamu mwingine yeyote, Mwanasosholojia aliimiss sana familia yake, rafiki zake, ndugu na jamaa kwa kipindi chote alichokuwa Dublin. Anakwenda nchi ya Kikwete akiwa na kumbukumbu kibao za Dublin na watu wake, waitwao kwa kidhungu Waairishi. Mwanasosholojia alipofika Dublin, alitamani kurudi baada ya wiki tu, kufuatia hali ya hewa ambayo haikuwa rafiki kwake...baridi lisilokwisha...snow ya nguvu na mvua! Alizoea joto la Bongo ati! Hata hivyo alipiga moyo konde na kuendelea na maisha...kubwa kuliko, kuitafuta elimu.

Si vibaya kama wadau wa Mwanasosholojia mkashea naye taswira mbalimbali alizopitia akiwa Dublin;


Hapa Mwanasosholojia akionesha kuwa naye wamo katika mazoezi ya hewani

Mtaa maarufu wa Henry, katikati ya jiji la Dublin. Mwanasosholojia alikuwa anapita hapa mara kadhaa

Huu mnara ulikuwa unamsaidia sana Mwanasosholojia alipokuwa akipotea mjini, ulimsaidia kumwonesha anapopandia basi kurudi chuoni!

Haya ni maandamano ya wafanyakazi Dublin, Mwanasosholojia aliwahi kuyashuhudia, yakamkumbusha Bongo, virungu vya mandata kwenda mbele, Dublin mambo mswano!

Mwanasosholojia (kulia) akiwa na rafiki zake tayari kwa msosi, hao wabongo alikuwa nao Dublin, huyo mtasha ni rafiki yake muitaliano anaitwa Giorgio

Mwanasosholojia akiwa amejipumzisha sebule aliyokuwa anaishi

Mlango wa chumba alichokuwa anaishi Mwanasosholojia

Hapa jamani wadau alikuwa anaigiza tu, si kweli...kukata gogo na nguo! Ila ni eneo maalumu alilokuwa akilitumia katika yale mambo yetu yaleeee...

Alipokuwa anaweka ubavu!

Chumbani kwake...kifaa hiki ndicho mara nyingi kilikuwa kinawaletea haya mambo bloguni

Alikuwa anaishi jengo hilo hapo juu ghorofa ya tatu...angalau aliishi ghorofani ati!

Hapa alikuwa anakwenda mara kwa mara kufua nguo

Dukani alikokuwa akinunua mara kwa mara mahitaji yake

Anaweza kuruka juu...si haba ati!

Akionesha lilipokuwa dawati lake...kaofisi kadogo!

Akipozi mbele ya kibao kinachoonesha ofisi za utafiti

Anapenda mifugo!

Akiwa na Kamarade Lupa...huyu jamaa wa karibu sana na Mwanasosholojia, yeye ni Mwanaelimu ya Siasa toka UDSM

Akipozi kimazoezi

Siku zote aliingia jikoni kurekebisha mambo!

Huenda mmeinjoi wadau...maoni yoyote?

7 comments:

  1. Mi binafsi nimezifurahia picha zako. Kikubwa ni kwamba nakutakia SAFARI njema na nakuomba usiache kublog. Kwani kuna mambo mengi nimejifunza katika blog yako. Salimia Familia yako na kula sana vyakula vya nyumbani. Ila nakuonea wivu ujue:-)

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru kwa picha nzuri,Raha sana kumuona mwanaume anaingia jikoni kupika,nakuonea wivu unaenda nyumbani,tunakutakia safari njema Mwenyenzi Mungu akutangulie.Mada zako zilizopita zinapatikana wapi?

    ReplyDelete
  3. Hello kaka,
    Hongera sana kwa kutupa habari kamili ambayo pamoja na picha basi ujumbe unakuwa umefika kikamilifu.

    Salaamu sana kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki pia nikutakie likizo njema huko Tanzania.

    Nakutakia mafanikio mema

    ReplyDelete
  4. Mambo yako kumbe mswano,
    Kuna vitu vinono nono,
    Blog yako imetulia.

    Karibu sana nyumbani,
    Umechoka ugenini,
    Likizo kujipumzikia.

    ReplyDelete
  5. Hongera.Mambo vipi?karibu Bongo tusaidiane kuyaweka mambo sawa, manake utofauti wa kimazingira utakauona na kufanya tathmini toka ulipoondoka na sasa, ndio huo utakusuma kusimamia mabadiliko.

    ReplyDelete
  6. Dada Yasinta Ahsante sana, sitaacha kublog!Una wivu...maskini usijinyonge dadangu, na wewe si ulikuwa Bongo hivi karibuni?

    Manka ahsante pia, jikoni ni kawaida kwangu, na wala sioni aibu mwanaume kuandaa maakuli..kupika si mwanamke tu..ni kazi ya wote! Mada unazoulizia ni zipi, za blog au za taaluma?Nijulishe nikufahamishe.

    kaka Mbilinyi ahsante, salamu zimefika...tupo pamoja siku zote!

    Mtanga ndugu yangu
    Pia Malenga wangu
    Unaugusa Moyo wangu
    Kunikaribisha nyumbani kwangu!

    Tram, nitakutafuta, wewe ni mtu muhimu. Tuendeleze libeneke!

    ReplyDelete
  7. ANGELA JULIUS05/10/2011, 10:33

    NITAKUPANDIA HUKO GHOROFANI UNAJUA UNANITAMANISHA IN SHORT MATUKIO YA PICTURE ZAKO UMEPANGALIA VIZURI KABISA.

    ReplyDelete