10/05/2009

Vimbwanga vya Uchaguzi Ulaya!

Wadau mnaiona hiyo? Hiki ni kipindi cha kampeni za chaguzi (Local Elections) nchini Ireland. Wagombea wanajinadi na kujipigia upatu ili kupewa libeneke la kuongoza raia. Moja ya mbinu wanayotumia ni kubandika picha zao na maelezo katika mabango barabarani. Katika pita pita zangu nimekutana na hiyo picha hapo juu nikaona si vibaya kuwashirikisha. Ukiitizama unagundua ya kuwa picha ya mgombea wa chini imegeuzwa chini juu hali inayopelekea ugumu hata kusoma maelezo yake.

Angalia zaidi hapa chini;

Sijui waliofanya hivi ni wapiga debe wa mgombea mwenye picha ya juu??

Moja ya mabango ya kujinadi ya wagombea katika mitaa ya Dublin

Kwetu bongo kipindi cha uchaguzi huwa tunashuhudia vimbwanga vya namna hii pia? Bongo wagombea huwa wanalalamikia wizi wa kura, sijajua kwa huku, labda tusikilizie!

4 comments:

 1. Kazi kwelikweli, labda walipoigeuza hiyo picha walimaanisha hawamtaki huyo haina maana ya kmpigia kura atoke tu

  ReplyDelete
 2. Hujambo Mathew?
  Kuna kazi inakusubiri. Pitia kwangu kwa maelezo.
  Serina.

  ReplyDelete
 3. Sijambo da Serina, nitapitia kuifanya hiyo kazi! Ahsante kwa kunitembelea!

  ReplyDelete
 4. Hiyo picha imeniacha hoi kabisa!!

  ReplyDelete