21/02/2010

Kusaidiana Majukumu!

Mdau amenitumia hii picha na kuomba niitundike hapa barazani huku akisisitiza "umuhimu wa kusaidiana majukumu". Mnaionaje hii wadau??

6 comments:

  1. Mimi binafsi nasema hii ni safi sana haya ndo maisha sio mwanamke afanye kila kitu. Nimeipenda sana hii Taswira. Safi sana!!

    ReplyDelete
  2. Hii sasa ni hasara. kwa sababu hapo inavoonekana hakuna kugawana majukumu, bali ni kudhalilishana. Feminism ya namna hii mimi sikubaliani nayo, japo mimi pia ni mwanamke.

    Picha kama hizi haziwezi kubadilisha chochote katika struggle ya wakinamama, kinchohitajika ni mapinduzi yakimawazo kwa wakina baba, na sio picha za kuweka jinsia moja juu na nyingine chini.

    ReplyDelete
  3. Kwa upande wangu naona ni vizuri sana kusaidiana majukumu sio vizuri mwanamke afanye kila kitu wakati mwanaume kakaa anaangalia TV.Mambo kusaidiana jamani!!

    ReplyDelete
  4. Huyu amekaliwa huyu. Kalishwa limbwata mpaka kawa ndodocha hajiwezi. Inabidi apelekwe kwa mganga akashughulikiwe....

    ReplyDelete
  5. Kwa sisi wabeba maboksi tulioko huku nje hii mbona tumeshazoea. Maisha yanaenda kasi na kila mtu yuko "bize". Inabidi kusaidiana. Kuna ridhiko fulani spesheli linalopatikana kutokana na kushirikiana katika malezi na kazi za nyumbani kama hizi. Na ukaribu wa kweli kati ya mtoto na babake unaojengeka kutokana na ushirikiano huu haupimiki. Mwanasosholojia, hebu ngoja nikapige deki ili mama akirudi akute nyumba inang'ara! Chakula kiko tayari...

    ReplyDelete
  6. sio wote wabeba box wapo hivyo labda na wewe na ukianzxa tabia hizo "FATHER" umekwisha usifikiri mwanamke atakuonea imani wapi!! ndio sasa anakuona bwege na anaweza kufanya jambo lolote, mara utasikia anamidume mengine ya pembeni, haogopi tena. kwa hiyo bwana msiwadekeze hivyo mademu.mdau Leiocester.uk

    ReplyDelete